Skip to main content

TMRC: imefanikiwa kuorodheshwa hatifungani yenye thamani ya bilioni I20

Kampuni ya mikopo ya nyumba (TMRC) imefanikiwa kuorodheshwa hatifungani yenye thamani ya bilioni I20 katika soko la hisa la Dar es Salaam (DSE) jambo ambalo litasaidia kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kutumia fursa zilizopo katika sekta ya masoko katika mitaji.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya kuorodhesha hatifungani za kampuni ya TMRC soko la hisa (DSE) Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe Dkt. Ashatu Kijaji, amesema kuwa hatua ya TMRC ni mkakati wa maksudi wa kutekeleza jukumu lake la msingi la kutafuta na kukuza mtaji kwa ajili ya kuinua sekta ya mikopo ya nyumba pamoja na mitaji.

"Hatifungani ya TMRC ni ya muda wa miaka mitano ambayo kitaalamu itaipatia kampuni fedha za kukopesha mabenki kwa ajili ya mikopo ya nyumba kwenye soko la fedha za ndani" amesema Dkt. Kijaji.

Amesema hatua hiyo itachangia kukua kwa masoko ya mitaji hapa nchini, kwani ni wakati mwafaka sekta ya fedha kuwa imara kwa kuendelea kuchachua ukuaji wa uchumi.

Dkt. Kijaji ameeleza kuwa kampuni ya TMRC katika utendaji wake imefanikiwa kutoa mikopo yenye thamani ya shillingi bilioni 91 kwa Benki I4 hapa nchini, huku watanzania 937 wakinufaika moja kwa moja na mikopo itolewayo.


Amesema wananchi 4,209 wamenufaika na mikopo ya nyumba kutokana na uwepo wa mfumo wa mikopo ya nyumba unaowezeshwa na TMRC.


''Katika kuhakikisha mikopo ya nyumba inaanzishwa serikali kwa kushirikiana na Benki ya dunia ilianzisha mradi wa kuwezesha kuwepo kwa mfumo wa mikopo ya nyumba (Housing Finance)'' amesema Dkt. Kijaji

Amefafanua kuwa katika kusaidia upatikanaji wa mikopo ya nyumba kwa gharama nafuu kwa kutumia teknolojia mbadala, mashirika kadhaa yamehusishwa ikiwemo shirika la nyumba la taifa (NHC), Shirika la Utafiti wa Ujenzi (NHBRA) pamoja na Watumishi Housing (WHC).

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) Nicodemus Mkama, ameipongeza bodi ya uongozi wa kampuni ya TMRC kwa kufanikisha uorodheshaji wa hatifungani ya katika soko la hisa.

Amesema kuwa kazi waliofanya haikuwa ndogo na rahisi kwani wamefanya kwa uweledi na kwa ufanisi mkubwa.

"Fedha zipatikanazo kupitia mauzo ya hatifungani zitatumika kugharamia shughuli za maendeleo ya kampuni ya TMRC pamoja na kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa benki  zinazotoa mikopo ya nyumba" amesema Mkama.

Mkama ameeleza kuwa kupitia hatifungani hiyo Kampuni itakuwa na uwezo mkubwa wa kupanga na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika kukuza sekta ya nyumba kufuatana na mpango wa biashara wa TMRC.

"Taasisi za fedha, bima na Kampuni zingine kutumia fursa zilizopo katika sekta ya masoko ya mitaji ili kupata fedha za kutekeleza miradi ya maendeleo" amesema Mkama.

Ametoa rai kwa wadau wa masoko ya mitaji kuendelea kushirikiana na serikali katika kutekeleza mipango ya kuendeleza mitaji ikiwemo kuleta bidhaa mpya ambazo zitaorodheshwa katika soko la hisa.

Kuorodheshwa kwa hatifungani katika soka la hisa ninakuwa ni jambo kubwa katika maendeleo ya masoko ya mitaji hapa nchini pamoja na ukanda wa afrika Mashariki, kwani kamapuni ya TMRC inakuwa ni hatifungani ya kwanza yenye muundo wa kudhaminiwa na mali  (Asset Backed Security-ABS).

Comments

Popular posts from this blog

Thousands of protesters clash with police in Chicago: Chaos in the Windy City as 45 activists arrested and one cop stabbed after demonstrators target NATO

By DAILY MAIL REPORTER Thousands of demonstrators upset with the war in Afghanistan, climate change and the erosion of union rights have raised the intensity of a march in downtown Chicago on Sunday as world leaders assembled for a NATO summit. The protest, one of the city's largest in years, turned violent at the end of an anti-NATO march, where demonstrators confronted Chicago police, pushing against a line of officers several blocks from the lakefront convention center where President Obama hosted a gathering of world leaders. Authorities were seen making arrests one by one and leading individual demonstrators away in handcuffs. After a clash near McCormick Place, Chicago Police Superintendent Garry McCarthy said at a news conference that the protests resulted in 45 people being arrested and four officers suffering injuries - one from a stab wound in the leg. Scroll down for video Clash: Demonstrators try to flee the police as they are move in on them ...

MBINU ZA KUMFIKISHA MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KILELENI KWA HARAKA

Kwa kawaida wanawake wanafikia kilele (mwisho wa utamu wa ngono) kati ya dakika ishirini na saa moja, yaani kwa kifupi inawachukua muda mrefu sana hali inayopelekea mpenzi mvivu kuchoka na ufanyaji wake utakuwa wa “ovyo” hali itakayo kufanya wewe kuishiwa na hamu ya kuendelea. Pamoja na kuchelewa huko ambako kunatokana na utofauti wetu kati ya mwanaume na mwanamke lakini nakumbuka hapo nyuma nilikutana na wanawake 2 waliokuwa ndani ya ndoa na wamezaa lakini hawajawahi kabisa kujua utamu wa tendo hilo alimaharufu kama “kufanya mapenzi”. Natambua kuwa ni ngumu au niseme si wanawake wote ambao wamejaaliwa kimaumbile kwamba wanafanikiwa kufika kileleni zaidi ya mara mbili kila wanapofanya mapenzi/ngono (kumbuka ni kati ya dakika 15 na saa moja hivyo Jibaba hapa awe na uwezo wa kujizuia kwa zaidi ya dk 45) na ikiwa jamaa ni “mzamiaji” basi unaweza ukaondoka na goli 3 ktk mzunguuko mmoja. Lakini kwa nini basi baadhi yao tu ndio wafike kileleni na wengine was...

LEO NI BUNGE LA BAJETI

Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo. -WANANCHI WATAKA IPUNGUZE UKALI WA MAISHA MACHO na masikio ya mamilioni ya Watanzania na wadau wa nje, leo yanaelekezwa Dodoma ambako Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2011/12 itasomwa.Wananchi wengi wamekuwa na shauku ya kujua mwelekeo wa bajeti hiyo hasa katika kipindi hiki ambacho wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha iliyotokana na kupanda kwa bei vyakula na bidhaa za mafuta. Kwa takriban wiki nzima iliyopita, baadhi ya wananchi wamekuwa wakituma ujumbe mfupi wa maandishi kwa simu katika vyombo vya habari, wakiisihi serikali kuhakikisha kuwa bajeti ya mwaka huu inawaondoa katika hali ngumu ya maisha. Bajeti hiyo itakayosomwa bungeni na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo itatangazwa kwa wakati mmoja na bajeti za serikali za nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), katika mtazamo wa kuimarisha mshimakano na umoja wa nchi hizo. Kwa kawaida na mazoea ya muda mrefu, baj...