WAKATI tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC)Agosti 12 ikiwa imetangaza kuwa
mwaka huu itakuwa ni siku ya uchaguzi mdogo wa ubunge katika jimbo la
Buyungu na wa madiwani katika kata 79 Tanzania Bara.
Jijini Dar es Slaam Katibu mwenezi wa Chama Cha MapinduziSimon
Mwakifwamba amesema jana kuwa (CCM)Mkoa wa Dar es Salaam
hupo katika maandalizi ya onesho kubwa litakarofanyika kwenye
viwanja vya jijini hapa.
Mwakifwamba alisema kuwa hali ya maandali hayo inaendelea vizuri na
tayari onesho hilo limepangwa kufanyika Julai 21 mwaka huu katika
viwanja hivyo na kikubwa ni kuwa bendi mbali mbali pamoja na wasanii
nyota akiwemo Nguza Viking 'Babu Seya' na Papii Kocha watatumbuiza.
"Lengo la siku hiyo ni kuwa wadau wote wa CCM watapata kukutana kwa
pamoja na kufahamiana kwa ukaribu hali itakayofanya waweze kubadilishana
mawazo kisiasa,"alisema Mwakifwamba .
Mwakifwamba alisema kuwa kumekuwa na namna nyingi za kufikishiana ujumbe
katika ngazi za uongozi CCM kuanzia ngazi ya kata hadi kitaifa sasa
tnaomba wanaumoja wote wakutane itakuwa vema sana kama kila mmoja akija
amempatia taarifa sahihi za kufika katika onesho hiulo mwenzake wa
karibu.
Aidha alisema kuwa CCM imekuwa katika mipango mizuri kiongozi na
uchapakazi wa kila mmoja unazaa malengo bora kwa taifa sasa ni bora
wakutane kwa pamoja kuamsha hisia njema za chama .
Pia aliwataja wasanii wengine watakao sherehesha siku hiyo kuwa ni
Juma Nature,Sharo Mwamba Dula Makabila,Segere Stars pamoja na wasanii
wengine nyota kama Christian Bella na Afande Sele kuota Morogoro.
Katika mchakato wa kunogesha onesho hilo bendi mahiri ya muziki wa Dansi
nchini Twanga Pepeta imepangwa kuburudisha onesho hilo sambamba na
Vijana Jazz ambapo milango ya kuingia katika onesho hilo imetanjwa kuwa
itakuawa wazi kuanzia saa 12:00 asubuhi hadi saa 06:00 usiku huku kiingilio
kikiwa bure.
Nyama choma na bia zitauzwa kwa gharama nafuu kabisa kama bei ya
uswahili kawaida.
Comments