WAFANYABIASHARA wa Kilimo nchini wametakiwa Shirika la Posta nchiniya Shirika la Posta nchini katika kutangaza bidhaa zao pamoja
na kuuza.
Hayo yamesemwa na Dar es Salaam jana na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi
Atashasta Nditiye alipofungua mkutano wa 16 wa
Mashirika ya Posta yaliyopo Nchi zilizo kusini mwa Afrika (SADEC), huku
akisisitiza kwa kufanya hivyo wafanyabiashara hao wataweza kuuza bidhaa
zao Dunia nzima.
''Unajua Shirika la Posta sasa hivi, linajulikana Dunia nzima, hivyo
wafanyabiashara kama watatumia website hii watapata fulsa ya kuonekana
dunia nzima, hali itakayopelekea kupata masoko makubwa ya Kimataifa'', alisema.
Alisema alisema kuwa, Shirika la Posta hivi sasa limehimarika linajiaendesha
kwa faida, hivyo lina uwezo wa kusafirisha vifurushi popote Duniani na mzigo
wako ukafika salama na pesa yako ukaipata bila matatizo.
Naibu huyo amezitaka taasisi zote za Serikali kulitumia Shirika hilo, katika
kusafirisha vifurushi ili kuliongezea uwezo liweze kuendelea kujiendesha kwa
faida ili liweze kutoa gawiwo kwa Serikali kila mwaka.
Nditiye aliongeza kuwa, wanatarajia kurekebisha baadhi ya sheria zilizokuwa
zikionekana kuwabana wateja, ili kwenda na wakati kwani mambo ya teknolojia
yamekuwa kwa kasi.
Aidha alisema kuwa, katika kuboresha huduma zao, Shirika la Posta
limeanzisha huduma ya Posta mlangoni ambayo tayari imeshaanza katika Mikoa
ya Dar es Salaam, Arusha na Dodoma.
Pia alisema shirika la Posta Tanzania tangu lizinduwe huduma
mpya POSTA MLANGONI limeendelea kuimalisha huduma hiyo katika jiji
la Dar es Salaam ambapo kila mwananchi atapelekewa kufurushi,
taarifa au bidhaa zilizotumwa kwa kupitia Ofisi za Posta kwa sasa
wameshatoa taarifa kwa madiwani,wawasiliane na watendaji wa Serikali
za mitaa,ili wapeleke majina ya mitaa yao Makao Makuu ya Posta,ili
zoezi hilo likamilike wananchi waweze kupelekewa barua au vifurushi
vyao mpaka mlangoni mwao.
''Lengo la Posta Mlangoni ni kuenea Tanzania nzima, isipokuwa kwa sasa
tumeanza na hii Mikoa mitatu, hivyo wananachi wasubiri wapatatiwa huduma
hiyo kwa kufuatwa majumbani mwao'', alisema.
Mkutano huo wa 16, una lengo la kujadili mambo mbali mbali yahusuyo Posta,
pamoja na kujadilianani jinsi gani wataweza kuimarisha huduma zao ili ziweze
kufanyika kwa ufanisi mkubwa.
Naye mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC),
Luteni Kanali mstaafu, Dk. Haroun Kondo alisema kuwa mkutano huo kufanyika
hapa nchini unaweza kutafuta pia fursa za kuboresha huduma kama mambo ya
kiteknolojia.
Comments