Pichani
wapili kutoka kushoto Dkt.Ambege Mwakatobe akikata utepe katika
ufunguzi wa Similes Dental Clinic iliyopo mtaa wa Jamuhuri Dar es
Salaam.
Akizungumza Dar es Salaam katika Mtaa wa Jamhuri wakati wa uzinduzi
wa Kliniki mpya ya Similes Dental itakayokuwa inatibu ugonjwa huo wa
kinywa Dkt. Ambege Mwakatobe alisema kuwa asilimia 80 ya watu wazima
duniani wanasumbuliwa na ugonjwa wa kuumwa fizi.
wa Kliniki mpya ya Similes Dental itakayokuwa inatibu ugonjwa huo wa
kinywa Dkt. Ambege Mwakatobe alisema kuwa asilimia 80 ya watu wazima
duniani wanasumbuliwa na ugonjwa wa kuumwa fizi.
Alisema kuumwa na fizi kunaweza kusababisha kuumwa ugonjwa wa moyo
ambapo hali nyingine ya ugonjwa huo wa meno unaweza kusababishwa
na unywaji pombe kupindukia.
"Unywaji wa pombe kupindikia ni miongoni mwa hatari zinazo
weza kuchangia kuweza kupata matatizo ya ugonjwa wa meno,
ambapo matatizo yab ugonjwa wa meno mtu akiwa na mate madogo
uweza kupata ugonjwa huo kwani mate pia usaidia kulinda meno
katika kinywa,"alisema Dkt.Mwakatobe.
Alibainisha kuwa wamejipanga vema kutoa huduma ya tiba ya wagonjwa
ya meno ambapo gharama yao ni nafuu watu wenye matatizo ya meno wasisite
kufika kliniki hiyo na kwamba wapo mbioni kuanza kutoa huduma hiyo ya
tiba kwa watu wenye bima za afya.
Alieleza kuwa tatizo la ugonjwa wa meno linachangiwa pia na sababu ya
vyakula vyenye mafuta ama vitu vyenye mafuta kwa mtumiaji wa vitu hivyo,
pamoja na upande mwingine wa utumiaji wa vitu kama sukari.
Aidha alisema kuwa magonjwa ya saratani ya meno husababishwa na utumiaji
wa tumbaku na kuongeza kuwa magonjwa ya kinywa ni hatari kwa mama mjamzito
kwani endapo ataumwa fizi ni rahisi kupata ugonjwa wa moyo.
"Nawashauri watu kuchunguza afya zao za kinywa angalau mara moja
kwa mwaka hili kugundua matatizo yanayoweza kujitokeza siku za mbeleni,"
alisema Dkt.Mwakatobe .
kwa mwaka hili kugundua matatizo yanayoweza kujitokeza siku za mbeleni,"
alisema Dkt.Mwakatobe .
Alisisitiza kuwa kwa sasa madaktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
wametaja kuwa asilimia 50 ya watoto wenye rika la kwenda shule ndio
hasa waanga wa ugonjwa wa meno.
wametaja kuwa asilimia 50 ya watoto wenye rika la kwenda shule ndio
hasa waanga wa ugonjwa wa meno.
Comments