Wizara ya Afya:Yahimiza kuhamasisha na kuongeza uelewa wa jamii kuhusu humuhimu wa lishe bora kwa watoto
AZIRI wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kesho Tanzania inaungangana na nchi zingine duniani kuadhimisha wiki ya unyonyeshaji wa maziwa ya mtoto.
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Ummy leo alisema Kila mwaka kuanzia Augosti mosi maadhimisho hayo yamekua yakifanyika na
kupewa kaulimbiu maalum zinazolenga kuhamasisha na kuongeza uelewa
wa jamii kuhusu humuhimu wa lishe bora kwa watoto na taratibu sahihi
za ulishaji.
Alisema siku 100 za mwanzo wa uhai wa matoto ni kipindi muhimu cha kujenga msingi wa maisha ya mtoto hususani maendeleo ya ukuaji wake
kimwili na kiakili.
"Siku hizo mtoto huanza kuhesabiwa tangu pale mimba inapotungwa hadi mtoto anapotimiza umri wa miaka miwili nakuwa mtoto anapohitaji kunyonyeshwa anyonyeshwe wakati anapoitaji iwe usiku ama mchana,"alisema Ummy .
Waziri Ummy alisema kuwa katika hatua ya ujauzito mtoto ana tegemea chakula anachopata mama yake ambapo mama akipata chakula sahihi vivyo hivyo mtoto atapata virutubisho sahihi.
Alisema iwapo mama mjamzito mlo ambao ni duni hali hiyo pia itamkumba mtoto aliye tumboni,mtoto akisha zaliwa chakula chake cha awali na cha msingi ni maziwa ya mama yake pekee.
Ummy alieleza kuwa tendo la kunyonyesha humsaidia mama kupangilia uzazi,kupunguza uwezekano wa kupata saratani ya matiti na via vya uzazi na kuzuia upotevu wa kiwango kikubwa cha damu baada ya kujifungua.
Wizara ya afya inaeleza kuwa maziwa ya mama humpatia mtoto kinga ya
mwili zinazosaidia kupambana na maambukizo ya magonjwa kupunguza kasi
ya kuugua mara kwa mara hususani ugonjwa wakuharisha,maambukizi kwenye
mapafu pamoja na masikio.
Wizara hiyo pamoja na Taasisi ya Chakula na Lishe na UNISEFU zimesisitiza kuwa mzazi asimpe mtoto maji au chakula kingine kile ndani ya miezi sita na kuwa ikumbukwe maziwa ya mama yana
virutubishi vinavyohitajika kwa ukuaji wa mtoto.
Wkati siku leo Tanzania inaungangana na nchi zingine duniani kuadhimisha wiki ya unyonyeshaji wa maziwa ya mtoto imebainika kuwa asilimia 100 ya watoto nchini asilimia 30 ya watoto imedumaa.
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetaja
kuwa mikoa inyoongoza kwa kuwa na wingi wa watoto wenye udumavu
kuwa ni Mkoa wa Rukwa ukiwa na asilimia 50 huku Geita ukiwa na asilimia
40 na Mkoa wa Kagera na Iringa ukiwa umetajwa kuwa na asilimia 41.
"Jambo la ajabu kuona mikoa iliyotajwa kuongoza kwa udumavu ndio inayokuwa na mvua nyingi na rutuba kuliko ata mikoa yenye ukame,"alisema Ummy.
Comments