Wizara ya Afya:Yahimiza kuhamasisha na kuongeza uelewa wa jamii kuhusu humuhimu wa lishe bora kwa watoto
AZIRI wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kesho Tanzania inaungangana na nchi zingine duniani kuadhimisha wiki ya unyonyeshaji wa maziwa ya mtoto. Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Ummy leo alisema Kila mwaka kuanzia Augosti mosi maadhimisho hayo yamekua yakifanyika na kupewa kaulimbiu maalum zinazolenga kuhamasisha na kuongeza uelewa wa jamii kuhusu humuhimu wa lishe bora kwa watoto na taratibu sahihi za ulishaji. Alisema siku 100 za mwanzo wa uhai wa matoto ni kipindi muhimu cha kujenga msingi wa maisha ya mtoto hususani maendeleo ya ukuaji wake kimwili na kiakili. "Siku hizo mtoto huanza kuhesabiwa tangu pale mimba inapotungwa hadi mtoto anapotimiza umri wa miaka miwili nakuwa mtoto anapohitaji kunyonyeshwa anyonyeshwe wakati anapoitaji iwe usiku ama mchana,"alisema Ummy . Waziri Ummy alisem...