Skip to main content

Yule Bilionea Dangote akagua ujenzi wa kiwanda chake cha saruji Mtwara


Bilionea mwenye dola nyingi kuliko wote barani Afrika, Alhaj Aliko Dangote kutoka Nigeria amefanya ziara mkoani Mtwara kukagua hatua zinazopigwa katika ujenzi wa kiwanda chake kikubwa cha saruji mjini Mtwara.
Kasi ya kazi hiyo ni kubwa na kitapomalizika kitaongeza kiwango cha saruji inayozalishwa nchini kwa kiasi cha tani milioni tatu kwa mwaka.
Bilionea kutoka Nigeria ambaye ni Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Dangote Group of Industries, Alhaj Aliko Dangote (kulia) akiteremka kwenye ndege alipowasili Mtwara, kwenda kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanda chake kikubwa cha saruji kinachojengwa mkoani humo.
Msafara wa Alhaj Dangote ukipita eneo la kiwanda kukagua shughuli inavyopiga hatua.
Kiwanda hicho kinatarajiwa kuchangia kukuza upatikanaji wa ajira mkoani Mtwara na kukuza uchumi. Vile vile kupunguza gharama za upatikanaji wa saruji maeneo ya kusini mwa Tanzania na nchi jirani.

Comments