Ikulu ya
white house nchini Marekani inasema kuwa rais Brack Obama amemteua
mwendesha mashtaka wa mji wa New York Loretta Lynch kuwa mkuu wa sheria
nchini humo.
Msemaji wa ikulu ya white house alisema kuwa mkuu huyo mpya wa sheria atateuliwa rasmi leo Jumamosi.
Ikiwa
uteuzi wake utaidhinishwa na bunge la seneti Loretta Lynch atakuwa
mwanamke wa kwanza mwenye asili ya afrika kuwa mkuu wa sheria nchini
marekani .
Uteuzi
huo unafanyika wiki sita baada ya kujiuzulu kwa Eric Holder ambaye ndiye
M'marekani wa kwanza mweusi kuteuliwa kuwa mkuu wa sheria nchini humo.BBC (V.S)
Comments