Marekani
imesema itapeleka rasimu ya maazimio ndani ya Baraza la usalama la
Umoja wa Mataifa kuweka vikwazo dhidi ya Watu wanaozorotesha hali ya
kisiasa nchini Sudani Kusini.
Rais wa Baraza la usalama la Umoja
wa Mataifa ambaye ni Rais wa Australia amesema baadhi ya wanachama wa
baraza hilo wanaunga mkono hatua ya kuwekewa vikwazo na kuzuia biashara
ya silaha.
Haijajulikana ni lini hatua hiyo itatekelezwa.
Mapigano
yameendelea nchini Sudani Kusini ,ingawa kumekuwa na jitihada za
kimataifa kuhakikisha makubaliano ya amani yanatekelezeka.
Mzozo
wa kuwania madaraka uliokuwepo kwa miezi kumi kati ya Rais Salva Kiir
na aliyekuwa Makamu wake Riek Machar umegharimu maisha ya maelfu ya Watu
na takriban watu milioni mbili kuyakimbia makazi yao.
Makubaliano ya amani yaliyotiwa saini yalishindwa, kwa kuwa pande zinazokinzana zilishindwa kuunda Serikali ya umoja.BBC
Comments