Stori: Gladness Mallya
GOOD news
kwa mtoto mzuri Bongo Movies, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ ni kwamba
anatarajia kuolewa hivi karibuni baada ya kuishi maisha ya upweke kwa
muda mrefu, Risasi Jumamosi linakujuza.
Msanii wa Bongo Movies, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’.
Batuli
ambaye ni mama wa watoto wawili, ameliambia Risasi Jumamosi kuwa kwa
umri alionao, amejifunza vitu vingi katika maisha hivyo kwa kuwa
ameshampata mtu sahihi kwake, ameona bora aolewe.GPL(P.T)
Alisema
katika safari ya maisha, vikwazo ni vingi ikiwemo masuala ya skendo za
wasanii lakini ameshavuka vikwazo hivyo na hahitaji tena kuyumbishwa na
mtu kwani anaingia kwenye ndoa akiwa ameshajifunza mengi.
“Ndoa
siyo kitu cha mchezo tena kwa sisi wasanii mambo ni mengi. Kazi yetu
tunakutana katika mazingira mbalimbali hatarishi na wadau tofauti,
vikwazo ni vingi na mtu akivuka salama basi ni jambo la kumshukuru
Mungu,” alisema Batuli.
Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ akipozi.
Paparazi
wetu alimbana zaidi Batuli ili aweze kujua hiyo ‘hivi karibuni’ kwake
ina maana ya lini ambapo hakutaka kutaja tarehe ya harusi lakini
akaahidi kumwanika mume wake mtarajiwa Desemba 5, mwaka huu sambamba na
kutaja siku husika ya ndoa.
“Wewe
usijali, utakuwa wa kwanza kualikwa. Tena Desemba 5 nitakuita umuone
mume wangu mtarajiwa, nitakutambulisha kwa majina na kila kitu, baada ya
hapo nitakupa tarehe kamili ya ndoa yangu maana kila kitu kimeshakaa
kwenye mstari, soon tu nitakuwa mke wa mtu,” alisema Batuli.
Watoto
wawili ambao Batuli anao kwa sasa, alizaa na wanaume wawili tofauti
ambao hapendi kuwazungumzia kwa kuwa tayari zama zao zilishapita.
Comments