Skip to main content

GHARAMA MPYA ZA MUHIMBILI ZASITISHWA


SERIKALI imesitisha ongezeko la tozo zilizoanza kutumika hivi karibuni katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), ambayo ndiyo yenye vifaatiba na madaktari wenye uwezo mkubwa kuliko hospitali yoyote nchini.
Hatua hiyo ya Serikali, ipo katika kauli ya Serikali bungeni, iliyotolewa jana na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Seif Rashid, ambapo pia Bohari ya Dawa (MSD) iliagizwa kupeleka dawa muhimu zenye thamani ya Sh milioni 200 katika hospitali hiyo.
Hivi karibuni hospitali hiyo ilipandisha gharama za huduma hospitalini hapo, ambapo mgonjwa aliyetakiwa kulazwa baada ya kupatiwa rufaa kutibiwa katika hospitali hiyo, alipaswa kulipa Sh 5,000 kwa siku na Sh 2,000 za chakula, ambazo hazikuwepo hapo awali.
Taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, , ilikaririwa na vyombo vya habari, ikieleza kuwa gharama mpya zilianza kutumika Oktoba 17, mwaka huu.
Kutokana na gharama hizo, baadhi ya wahudumu hospitalini hapo walikaririwa wakisema idadi ya wagonjwa imepungua wodini kutokana na wengi wao kushindwa kumudu gharama.
Wagonjwa kutoka mikoani waliathirika zaidi, kwa kulazimika kutafuta malazi nje ya hospitali hiyo, hata kama hali zao ni mbaya.
Aidha, baadhi ya wananchi waliokuwa wakiuguza ndugu zao, walikaririwa kuchukua uamuzi wa kuwarejesha nyumbani ili kukwepa gharama hizo.
Miundombinu
Mbali na kusitisha ongezeko hilo la tozo, Dk Seif pia ameagiza uongozi wa hospitali hiyo kurekebisha mara moja mazingira na miundombinu ya hospitali hiyo, ambayo yapo ndani ya uwezo wao.
Ingawa tamko hilo halikufafanua, lakini taarifa zinaonesha kuwa hospitali hiyo ilikuwa ikizidiwa na wagonjwa, kiasi cha baadhi kulazimika kulala sakafuni.
Vyombo vya habari viliripoti kuhusu hali ya usafi wa vyoo vya wodi ya Sewa Haji kuwa mbaya, licha ya kuwapo taarifa za kutolewa kwa zabuni kwa kampuni kadhaa kufanya usafi, unaokidhi viwango na kanuni za afya bora.
Baadhi ya vyoo havikuwa na maji na vifaa vya kusukuma maji havikuwa vikifanya kazi, huku baadhi ya mabomba yakiwa na kutu.
Kutokana na ukosefu wa maji, wagonjwa na watu wanaowatembelea, alilazimika kutumia maji yaliyopo kwenye mapipa nje ya vyoo na yalipokosekana, walitafuta mahali kwingine ikiwamo nje ya jengo hilo.
Baadhi ya vyombo vya habari, viliripoti kushuhudia baadhi ya vyoo vikiwa vimejaa uchafu katika majengo ya Sewa Haji, Kibasila na Mwaisela huku vingi vikiwa katika hali mbaya ya uchakavu, kutokana na kutumika muda mrefu bila kufanyiwa ukarabati.
Deni MSD
Kuhusu deni la Bohari Kuu ya Dawa (MSD), Dk Rashid alisema Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha ilifanya uhakiki wa deni la MSD la Sh bilioni 41.5.
Baada ya deni hilo kuhakikiwa, alisema Serikali ilianza kulipa kwa awamu ambapo Sh bilioni 8 zililipwa Juni 14, Sh bilioni 2 Agosti na Sh bilioni 20 zimelipwa mwezi huu. Alisema kiasi kilichobaki cha Sh bilioni 11.5, kitalipwa mwezi ujao.
Kuhusu kutenga fedha za kununua dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi kupitia MSD ili kuhakikisha jamii ya Watanzania inapata dawa na vifaa tiba kwa wakati, alisema katika mwaka wa fedha wa 2014/2015, Bunge liliidhinisha Sh bilioni 70.5 kwa ajili ya kazi hiyo. Ocean Road Akizungumzia huduma za afya katika Hospitali ya Ocean Road, alisema huduma za matibabu ya saratani inaendelea kutolewa,
kutokana na mashine ya E80 kuendelea kufanya kazi na kwa sasa ndiyo inayotibu wagonjwa wote wa saratani katika taasisi hiyo.
"Kutokana na kuwepo kwa mashine moja tu ya mionzi inayofanya kazi, kwa sasa hivi mashine inafanya kazi kwa saa 18 kwa siku ili kupunguza mlundikano wa wagonjwa.
"Mashine ya intra cavitary ambayo ilikuwa imesimama kufanya kazi kutokana na ubovu na kukosekana kwa vifaa muhimu, imetengenezwa na sasa imeanza kufanya kazi hivyo kuwezesha matibabu ya wagonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi kwa ufanisi zaidi," alisema Waziri.
Nafasi ya Njelekela yatangazwa
Wakati hali ikiwa hivyo, nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, ilitangazwa jana kuwa iko wazi. Sifa za mtu anayetakiwa kujaza nafasi hiyo ni pamoja na Shahada ya Uzamili katika Udaktari wa Binadamu; au sifa inayolingana na hiyo katika masuala ya udaktari na upasuaji, pamoja na uzoefu wa zaidi ya miaka kumi katika uongozi wa hospitali.
Tangazo hilo lilitolewa na hospitali hiyo na lilikuwa katika gazeti la Daily News la jana, Ukurasa wa Nne. Waombaji wenye vigezo vinavyotakiwa, wanatakiwa watume maombi ya kazi hiyo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Hospitali.CHANZO:BONGO LEAKS

Comments

Popular posts from this blog

MBINU ZA KUMFIKISHA MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KILELENI KWA HARAKA

Kwa kawaida wanawake wanafikia kilele (mwisho wa utamu wa ngono) kati ya dakika ishirini na saa moja, yaani kwa kifupi inawachukua muda mrefu sana hali inayopelekea mpenzi mvivu kuchoka na ufanyaji wake utakuwa wa “ovyo” hali itakayo kufanya wewe kuishiwa na hamu ya kuendelea. Pamoja na kuchelewa huko ambako kunatokana na utofauti wetu kati ya mwanaume na mwanamke lakini nakumbuka hapo nyuma nilikutana na wanawake 2 waliokuwa ndani ya ndoa na wamezaa lakini hawajawahi kabisa kujua utamu wa tendo hilo alimaharufu kama “kufanya mapenzi”. Natambua kuwa ni ngumu au niseme si wanawake wote ambao wamejaaliwa kimaumbile kwamba wanafanikiwa kufika kileleni zaidi ya mara mbili kila wanapofanya mapenzi/ngono (kumbuka ni kati ya dakika 15 na saa moja hivyo Jibaba hapa awe na uwezo wa kujizuia kwa zaidi ya dk 45) na ikiwa jamaa ni “mzamiaji” basi unaweza ukaondoka na goli 3 ktk mzunguuko mmoja. Lakini kwa nini basi baadhi yao tu ndio wafike kileleni na wengine was...

Uganda Police issue fresh terror alert

  By Chris Kiwawulo, The Police have issued a fresh terror alert against a possible attack on Uganda by four terrorists from Kazakhstan. Police spokesperson Judith Nabakooba “We have received a security notification in form of an orange notice of four terrorists originating from Kazakhstan who are planning to travel to foreign countries in order to commit attacks and participate in hostile acts,” Police spokesperson Judith Nabakooba said in a statement on Monday. Nabakooba named the four active members of radical organizations as; Nassiruauly Kairat, Umurzakov Marat Eskendirovich, Kovtun Denis Valerevich and Mazhibayen Alimzhan Akhlazhanovich. By press time, a search on the international web has not yielded anything on the named persons.Last evening, police said that in collaboration with other security agencies vigilance has been stepped up to avert the terrorists’ evil plans. Police have in the past issu...

Poland’s GROM special services mastermind found dead

Brigadier General Slawomir Petelicki, responsible for the formation of the GROM special services unit in the 1990s, was found dead at his apartment, Saturday, with bullet wounds to the head. Sławomir Petelicki, 1946-2012. Photo: Archive/PAP/Radek Pietruszka Police spokesman Maciej Karczynski informed that Petelicki’s body was found by his wife in the garage of his Warsaw apartment on Saturday. He was 65. Primary investigations point to suicide as the cause of death. It is expected that prosecutors will decide on an investigation into Petelicki’s death on Monday. After examining the scene of the incident, “the body of General [Petelicki] has been taken to a forensic laboratory, although a post-mortem will probably take place on Monday,” prosecutor Katarzyna Calow-Jaszewska from the Warsaw District Prosecution told the PAP news agency. “He was a tough man, a brilliant soldier and commander,” Colonel Krzysztof Przepiorka, head of the ...