Miss Tanzania Sitti Mtemvu, amejivua taji lake jana Jiji Dar es Salaam, kwa kuuandikia barua uongozi wa uandaaji wa mashindano hayo kampuni ya Lino International Agency, baada ya uvumi uliodai kuwa alidanganya umri wa kuzaliwa kwa kupeleka cheti kisicho sahihi na kudaiwa kuwa na mtoto.
Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ukumbi wa Jb Belmont, Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Hashimu Lundenga, alisema kuwa uwamuzi huo umefanywa baada ya Miss huyo kuwaandikia barua ya kujivua taji hilo kwa madai kuwa analinda heshima yake.
"Sitty ameamua kujivua taji hilo mwenyewe kwa madai kuwa analinda heshima yake kutokana na yale yaliyoongelewa siku mbili tatu za nyuma, na sisi hatuna budi kukubaliana na maamuzi yake kwani yeye ndiye muamuzi wa mwisho" alisema Lundenga.
Lundenga, alisema kuwa katika barua hiyo Sitty amewashukuru watu wote waliokuwa pamoja nae tangu hatua za awali hadi kufikia kuchukua taji la Miss Tanzani 2014.
"Sitty katika barua yake kawashukuru wale wote waliokuwa nae bega kwa bega tangu hatua za mwanzo hadi kuchukua taji lake, lakini pia katika barua hii kasema ingawa kalivua taji hilo lakini bado kabaki na taji lake lingine alilopewa na Mungu" alisema Lundenga.
Lundenga, baada ya kumaliza kusoma barua hiyo, alimtangaza rasmi Miss Mpya ambaye amechukua nafasi aliyokuwa Miss huyo na kusema kuwa kwanzia sasa Miss Tanzania ni yule aliyeshika namba mbili katika mashindano hayo lilian Deus (18), mwenye Cheti cha Udhamili alichokopata akiwa anasoma katika chuo kimoja cha Jijini Arusha.
"kutokana na sitti kujivua taji lake hivyo namtangaza rasmi Miss Tanzania 2014, ni Lilian Deus ambaye kataka mashindano hayo alishika nafasi ya pili, na Miss huyu ana umri wa miaka 18 na ametokea kanda ya Kaskazini" alisema Lundenga.
Sitti Mtemvu, kaamua kujivua taji lake baada ya kashfa ya kudaiwa kudanganya umri kwa pasipoti na leseni yake kutofautiana na umri wake huku kashfa nyingine akidaiwa kuwa na mtoto.

Comments