Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara
inaendelea wikiendi hii ambapo tiketi za elektroniki hazitauzwa tena
kwenye magari, hivyo washabiki wanunue tiketi hizo kwenye mtandao au
kwenye maduka ya CRDB Fahari Huduma.
Kesho (Novemba 8, 2014) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
kutakuwa na mechi kati ya Yanga na Mgambo Shooting wakati Uwanja wa
Chamazi kutakuwa na mechi kati ya Azam na Coastal Union. Jumapili ni
mechi kati ya Simba na Ruvu Shooting.
Viingilio kwenye mechi za Uwanja wa Taifa ni sh. 5,000 kwa viti vya
rangi ya kijani na bluu, sh. 8,000 (viti vya rangi ya chungwa), sh.
15,000 (VIP B na C) wakati VIP A itakuwa sh. 20,000. Mechi za Uwanja wa
Chamazi kiingilio ni sh. 3,000 kwa sh. 10,000.
Mechi nyingine za VPL kesho ni kati ya Stand United na Mbeya City
(Uwanja wa Kambarage, Shinyanga), Mtibwa Sugar na Kagera Sugar (Uwanja
wa Manungu, Morogoro).
Raundi hiyo ya saba itakamilika Jumapili kwenye Uwanja wa Chamazi,
Dar es Salaam kwa mechi kati ya JKT Ruvu na Ndanda kutoka Mtwara.
Wakati huo huo, mchezaji bora wa VPL kwa mwezi Oktoba, Salum Abubakar
wa Azam atakabidhiwa zawadi yake kesho kabla ya mechi kati ya Azam na
Coastal Union uwanja wa Azam Comple
Comments