Miguel Macedo waziri wa mambo ya ndani wa Ureno aliyejiuzulu
Waziri wa mambo ya ndani wa Ureno amejiuzulu kupisha uchunguzi kuhusu tuhuma za rushwa inayohusishwa na utoaji vibali vya mgawo wa makazi.
Miguel Macedo amesema hahusiki na kashfa hiyo lakini anajiuzulu kulinda heshima ya taasisi za serikali.
Polisi wamewakamata watu 11, akiwemo mkuu wa idara ya uhamiaji nchini humo, siku ya Alhamisi.
Ureno inatoa visa za daraja la kwanza kwa wageni wanaotaka kuwekeza nchini humo.
Mnufaika mkuu wa uharakishaji wa vibali ni raia wa China ambao wamekuwa wakiwekeza kiasi kikubwa nchini Ureno.
Polisi wamesema watu 11 waliokamatwa wanatuhumiwa kwa vitendo vya rushwa, fedha haramu, upendeleo na uhujumu uchumi.
Visa za daraja la kwanza au kwa tafsiri isiyo rasmi "visa za dhahabu" mpango huu uko wazi kwa wageni wanaowekeza kiasi kikubwa katika majengo na ardhi.
Bwana Macedo ameiambia serikali ya serikali kuwa "binafsi hahusiki na kashfa hiyo".
"Huu ni uamuzi unaozingatia, nafasi yake binafsi na uwajibikaji kisiasa," amesema.
"Nipo kutetea serikali na mamlaka za serikali na heshima ya taasisi."
Upekuzi ulifanyika katika maeneo kadha wiki iliyopita, ikiwemo wizara ya mambo ya ndani.
Manuel Palos, mkuu wa idara ya uhamiaji amehojiwa na jaji kwa tuhuma za kupokea rushwa, amesema mwanasheria wake.
Wakati huo huo, serikali ya Ureno imetetea mpango huo wa visa, ambao katika miaka miwili umeingiza nchini humo kiasi cha dola bilioni 1.3 za Kimarekani katika uwekezaji.BBC
Comments