Skip to main content

Kanda ya Ziwa yang’ara matokeo darasa la saba

 
Esther Mbussi na Adam Mkwepu, Dar es Salaam
SHULE za msingi katika mikoa ya Kanda ya Ziwa zimeongoza matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka 2014 kwa kushika namba moja hadi saba kati ya shule 10 bora kitaifa.
Aidha, watahiniwa wamefaulu zaidi somo la Kiswahili na kufeli zaidi somo la Hisabati.
Katika matokeo hayo yaliyotangazwa jana na Baraza la Mitihani la Taifa (NACTE), wavulana wameongoza somo la Hisabati kwa kupata alama 50/50, ambapo 26 wamefaulu kwa kiwango hicho na wasichana wakiwa wanane.
Akitangaza matokeo hayo, Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Charles Msonde, alizitaja shule 10 bora kuwa ni Twibhoki ya Mara ambayo imeshika nafasi ya kwanza, Mugini iliyoshika nafasi ya pili, Peace land na Alliance zote za Mwanza, Kwema (Shinyanga), St. Severine (Kagera), Rocken Hill (Shinyanga), Tusiime (Dar es Salaam), Imani (Kilimanjaro) na Palikas (Shinyanga).
"Kwa upande wa mikoa iliyofanya vizuri kitaifa na asilimia zake za ufaulu kwenye mabano ni Dar es Salaam (46,434), Kilimanjaro (26,192), Mwanza (37,017), Iringa (14,650), Arusha (23,250), Tanga (26,261), Njombe (11,389), Kagera (24,501), Geita (17,560) na Mtwara (15,608).
"Wilaya zilizoongoza kitaifa ni Mpanda Mji (Katavi), Biharamulo (Kagera), Moshi (Kilimanjaro), Kibaha (Pwani), Arusha (Arusha), Kinondoni (Dar es Salaam), Korogwe Vijijini (Tanga), Ilala (Dar es Salaam), Iringa (Iringa) na Mji Makambako (Njombe)," alisema Dk. Msonde.
Akizungumzia ufaulu wa kimasomo, alisema katika masomo yote umepanda kwa asilimia kati ya 0.64 na 8.94 ikilinganishwa na mwaka jana.
"Watahiniwa wamefaulu zaidi somo la Kiswahili ambapo ufaulu ni asilimia 69.70 tofauti na asilimia 69.06 ya mwaka jana, na somo walilofaulu kwa kiwango cha chini zaidi ni Hisabati lenye ufaulu wa asilimia 37.56 ambapo mwaka jana ilikuwa ni asilimia 28.62.
"Katika somo la Kiingereza watahiniwa waliofaulu kwa mwaka huu ni asilimia 38.84 ikilinganishwa na mwaka jana asilimia 35.52 na Sayansi kwa mwaka huu waliofaulu ni asilimia 54.89 na mwaka jana asilimia 47.49," alisema.
Dk. Msonde alisema jumla ya watahiniwa 451,392 kati ya 792,118 waliofanya mtihani huo wamepata alama 100 au zaidi katika alama 250 ambapo idadi hiyo ni sawa na asilimia 56.99.
Alisema kati ya watahiniwa hao, wasichana ni 226,483 ambao ni sawa na asilimia 53.59 na wavulana ni 224,909 sawa na asilimia 60.87.
Miongoni mwa watahiniwa hao waliofaulu, Dk. Msonde alisema wamo wenye ulemavu 795 wakiwamo wasichana 355 ambao ni sawa na asilimia 44.65 na wavulana 440 ambao ni sawa na asilimia 55.35.
"Katika mtihani huo uliofanyika Septemba 10 na 11, mwaka huu jumla ya watahiniwa 808,085 wa shule za msingi walisajiliwa kufanya mtihani huo wakiwamo wasichana 429,624 sawa na asilimia 53.17 na wavulana 378,461 sawa na asilimia 46.83.
"Kati ya watahiniwa hao waliosajiliwa, watahiniwa 691 walikuwa na uoni hafifu, 87 walikuwa na ulemavu wa macho (wasioona), wenye matatizo ya kusikia 374, wenye mtindio wa ubongo 252 na watahiniwa 27 walikuwa na ulemavu zaidi ya mmoja," alisema Dk. Msonde.
Pamoja na mambo mengine, NECTA imemfutia matokeo mtahiniwa mmoja aliyebainika kufanya udanganyifu katika mtihani huo. Mwaka jana watahiniwa 13 walifutiwa matokeo yao kwa kufanya udanganyifu.
Hata hivyo, Baraza hilo limesita kutoa matokeo ya shule zilizofanya vibaya kwa madai ya kuendelea na uchambuzi wa kuzitambua zaidi.

Comments

Popular posts from this blog

Thousands of protesters clash with police in Chicago: Chaos in the Windy City as 45 activists arrested and one cop stabbed after demonstrators target NATO

By DAILY MAIL REPORTER Thousands of demonstrators upset with the war in Afghanistan, climate change and the erosion of union rights have raised the intensity of a march in downtown Chicago on Sunday as world leaders assembled for a NATO summit. The protest, one of the city's largest in years, turned violent at the end of an anti-NATO march, where demonstrators confronted Chicago police, pushing against a line of officers several blocks from the lakefront convention center where President Obama hosted a gathering of world leaders. Authorities were seen making arrests one by one and leading individual demonstrators away in handcuffs. After a clash near McCormick Place, Chicago Police Superintendent Garry McCarthy said at a news conference that the protests resulted in 45 people being arrested and four officers suffering injuries - one from a stab wound in the leg. Scroll down for video Clash: Demonstrators try to flee the police as they are move in on them

MBINU ZA KUMFIKISHA MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KILELENI KWA HARAKA

Kwa kawaida wanawake wanafikia kilele (mwisho wa utamu wa ngono) kati ya dakika ishirini na saa moja, yaani kwa kifupi inawachukua muda mrefu sana hali inayopelekea mpenzi mvivu kuchoka na ufanyaji wake utakuwa wa “ovyo” hali itakayo kufanya wewe kuishiwa na hamu ya kuendelea. Pamoja na kuchelewa huko ambako kunatokana na utofauti wetu kati ya mwanaume na mwanamke lakini nakumbuka hapo nyuma nilikutana na wanawake 2 waliokuwa ndani ya ndoa na wamezaa lakini hawajawahi kabisa kujua utamu wa tendo hilo alimaharufu kama “kufanya mapenzi”. Natambua kuwa ni ngumu au niseme si wanawake wote ambao wamejaaliwa kimaumbile kwamba wanafanikiwa kufika kileleni zaidi ya mara mbili kila wanapofanya mapenzi/ngono (kumbuka ni kati ya dakika 15 na saa moja hivyo Jibaba hapa awe na uwezo wa kujizuia kwa zaidi ya dk 45) na ikiwa jamaa ni “mzamiaji” basi unaweza ukaondoka na goli 3 ktk mzunguuko mmoja. Lakini kwa nini basi baadhi yao tu ndio wafike kileleni na wengine was

HAYA NI MAKAO MAKUU YA MTANDAO WA Tigo TANZANIA DAR ES SALAAM

MAHALA yalipo ni Lugoda Street Gerezani Industrial Area , kwa sasa mdandao huu umefanya makubwa , kuna Tigo Bwerere Uilisha cheki hiyoooooo watu full kujiachia wana chonga tuu kwenye vyao vilonga.