Kwa
mara nyingine Chelsea imeonyesha ni moto wa kuotea mbali baada ya
kuifunga Liverpool 2 - 1 mbele ya mashabiki wao katika uwanja wa
Anfield.
Liverpool ndio waliokuwa wa kwanza kufunga goli
lililotiwa wavuni na Emre Can baada ya kupiga shuti na kumgonga beki
mmoja wa Chelsea na kujaa wavuni.
Baadae Chelsea wakaja juu na
kusawazisha goli kupitia kwa Gary Cahill baada ya mlinda mlango wa
Liverpool Simon Mignolet kuingia na mpira wavuni wakati alipokuwa
ameudaka. Goli la pili la Chelsea lilifungwa na Diego Costa kwa shuti
kali umbali wa takribani meta 15 ndani kisanduku cha 18.
Mechi
hiyo ya Chelsea na Liverpool katika uwanja Anfiled kunarejesha
kumbukumbu zisizofurahisha kwa upande wa Liverpool pamoja na hali yao ya
baadaye ambayo si nzuri sana.
Ni miezi sita tu ambapo
kuteleza kwa nahodha wa Liverpool Steven Gerard kuliisaidia Chelsea
kupata ushindi muhimu dhidi ya timu hiyo ya Mersyside, mechi ilioathiri
matokeo ya liverpool na ari yao ya kuwania taji la ligi hiyo msimu
uliopita.
Awali katika msimu uliopita mwishoni mwa mwezi Aprili
,kombe la ligi hiyo lilionekana likitaka kuelekea Liverpool lakini
baadae ndoto hiyo ilifutika kabisa.
Diego Coast alieanza katika
mechi dhidi ya Liverpool bado anaonekana ni moto wa kuotea mbali hasa
kwa bahati yake ya kufunga magoli.
Mchezaji huyo wa Uhispania
awali alikuwa akisumbuliwa na jeraha la paja na aliorodheshwa katika
kikosi dhidi ya Maribor katikati ya wili lakini hakucheza.BBC
Comments