Mkufunzi
wa timu ya Ivory Coast Herve Renard amewajumuisha wachezaji wa miaka
mingi Kolo Toure na Didier Zakora katika kikosi chake cha mechi za
kufuzu kwa dimba la bara Afrika mwaka 2015.
Wawili hao hawajashiriki katika mechi za kufuzu kwa dimba hilo kufikia sasa.
Timu
ya Ivory Coast ni ya tatu katika kundi D huku wakitarajiwa kuchuana na
Sierra Leone tarehe 14 mwezi Novemba na Cameroon siku tano baadaye.
Mechi
zote mbili zitachezwa mjini Abidjan kwa kuwa Sierra Leone haiwezi
kuandaa mchuano wao kutokana na mzozo wa ugonjwa wa ebola nchini mwao.
Hatahivyo hakuna nafasi ya mchezaji wa CSKA Moscow,Seydou Doumbia katika kikosi hicho cha wachezaji 24.
Mshambuliaji
huyo amefunga mabao sita katika ligi ya Urusi msimu huu ili kuisaidia
timu yake kukaa katika nafasi ya pili baada ya mechi 12.BBC
Comments