Marekani
imepinga madai ya taifa hilo kwamba imebadili sera zake dhidi ya Iran
kutokana na ripoti za magazeti na kuwa Rais Obama amekuwa na mawasiliano
ya siri na viongozi wa juu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei.
Jarida
la The Wall Street Journal lilitoa taarifa kwamba mwezi uliopita kuwa
Rais Obama alituma barua kwa Khamenei iliyobeba malengo ya pamoja katika
kupigana na kundi la wapiganaji wa kiislam la IS.
Msemaji wa Ikulu ya Marekani
White House Josh Earnest amepuuzakukanusha ama kukubali madai ya ripoti
hiyo dhidi ya Marekani kwamba sasa mlengo wake kwa Iran unalegezwa na
muungano wa kuungana pamoja kuwapiga kundi la IS.
Iran na mataifa mengine yenye nguvu Duniani ikiwemo Marekani yamekuwa yakijadiliana dhidi ya mpango wa Iran na Nyuklia.
Comments