Stori: Gladness Mallya GOOD news kwa mtoto mzuri Bongo Movies, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ ni kwamba anatarajia kuolewa hivi karibuni baada ya kuishi maisha ya upweke kwa muda mrefu, Risasi Jumamosi linakujuza. Msanii wa Bongo Movies, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’. Batuli ambaye ni mama wa watoto wawili, ameliambia Risasi Jumamosi kuwa kwa umri alionao, amejifunza vitu vingi katika maisha hivyo kwa kuwa ameshampata mtu sahihi kwake, ameona bora aolewe. GPL(P.T) Alisema katika safari ya maisha, vikwazo ni vingi ikiwemo masuala ya skendo za wasanii lakini ameshavuka vikwazo hivyo na hahitaji tena kuyumbishwa na mtu kwani anaingia kwenye ndoa akiwa ameshajifunza mengi. “Ndoa siyo kitu cha mchezo tena kwa sisi wasanii mambo ni mengi. Kazi yetu tunakutana katika mazingira mbalimbali hatarishi na wadau tofauti, vikwazo ni vingi na mtu akivuka salama basi ni jambo la kumshukuru Mungu,” alisema Batuli. Yobnesh Yusuf ‘Batuli’...