Na Editha Majura, Mwananchi
Dodoma. Siku moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kuzindua Bunge na kuponda
ripoti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji
Joseph Warioba amesema jukumu walilopewa kwa mujibu wa sheria
wamelikamilisha na wanawaachia wananchi waamue.
Jaji Joseph Warioba
Akizungumza na Mwananchi jana asubuhi, Jaji Warioba alisema
alichokizungumza Rais Kikwete ni maoni yake na kwamba hawezi kuyajadili.
“Rais Kikwete alichozungumza ni maoni yake, kwa sasa sipendi kuyazungumzia hayo, ” Jaji Warioba alieleza.
Alisema wamemaliza jukumu walilopewa na kwamba sasa jukumu lote lipo mikononi mwa Bunge.
Jaji Warioba alisema Tume yake ilikusanya maoni kutoka kwa wananchi,
mabaraza ya wilaya ya Katiba na Taasisi mbalimbali, wakatengeneza rasimu
ambayo sasa wameikabidhi kwa Bunge Maalumu la Katiba.
Jaji Warioba pia alikataa kuzungumzia zogo lililoibuka bungeni na
kusababisha rasimu kuwasilishwa Jumatano, baada ya kikao cha Jumanne
kuvunjika.
Comments