TAARIFA YA PINGAMIZI LA MGOMBEA WA UBUNGE JIMBO LA CHALINZE
FABIAN LEONARD SKAUKI – MGOMBEA CHAMA CHA WANANCHI – CUF
DHIDI YA
MATHAYO MANG’UNDA TORONGEY – MGOMBEA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO - CHADEMA
13.03.2014
Mimi FABIAN L. SKAUKI, mgombea ubunge wa uchaguzi mdogo jimbo la
CHALINZE kwa Ticket ya THE CIVIC UNITED FRONT (CUF) ninamwekea Pingamizi
mgombea wa chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwamba amepoteza
sifa za kuwa mgombea kwa sababu zifuatazo.
Ndugu MATHAYO. M. TORONGEY amejaza Taarifa za uongo kwenye Fomu yake kwamba kazi
anayoifanya ni BIASHARA. Sio kweli, kwa sababu hajaweka vielelezo vya yeye kufanya hiyo kazi. Hajulikani anafanya kazi gani.
Ndugu MATHAYO .M. TORONGEY amejaza katika fomu kwamba anajua kusoma na kuandika
Kiswahili na kiingereza. Taarifa hizi ni za uongo, mgombea huyu hajui
kusoma wala kuandika Kiswahili wala kiingereza, na kwamba amedanganya na
amepoteza sifa za kuwa mgombea.
Ndugu MATHAYO .M.TORONGEY amedanganya kwa kughushi/kufoji sahihi za
wadhamini,ambao amewaorodhesha kwenye fomu ya kuomba kuthibitishwa kuwa
mgombea. Ambapo katika fomu hizo wadhamini wote sahihi zao zimefojiwa na
hazifanani na zile zilizokuwepo kwenye daftari la kudumu la wapiga kura
na kwamba sahihi zote hizi zimesainiwa na mtu mmoja ambaye sio
muhusika. Hivyo anapoteza sifa ya kuendelea kuwa mgombea.
Comments