Star wa reality TV Khloe Kardashian
ameonekana katika jumba la kifahari la msanii Justine Bierber huko calabasas,califonia.
Habari
za uhakika zimesema kwamba mwanadada huyo ameinunua nyumba hiyo baada ya
kuwekwa mnadani na idara ya polisi ya eneo hilo tangu mwaka jana mwishoni kwa
sababu ambazo zimeelezwa kuwa Justine Bierber kushindwa kuishi vizuri na jirani
zake ikiwemo kuwasababishia majirani zake hasara ya dola za kimarekani $20 000
sawa na shilingi mil 32 za kibongo
Hakimu wa mahakama ya Los Angeles
kwa sasa anapitia ushahidi wa yote yaliyotokea na baadae ataamua endapo
atamfungulia mashtaka Justine Bierber.Meya wa Calabasas Fred Gaines amesema
usalama wa makazi ya watu ni kitu cha muhimu zaidi kwao na kwa bahati mbaya
wamekuwa na matukio mengi ya uvunjifu wa amani yanayomhusu Justine bierber na
makosa hayo yameelezwa wazi na idara ya
polisi ya eneo hilo
Justine(20) kwa sasa amepanga nyumba
Atlanta,Georgia akiwa na mpango kwa kununua nyumba hiyo na kuhamishia majeshi
pande hizo
Khloe amenunu mjengo huo kwa mkwanja
mrefu wa dola mil.7.5 za kimarekani sawa
na shillingi 12,000,000,000 (bil 12) za kibongo
Comments