Na Martha Magessa
Ili
kusaidia jamii kuondokana na adui umasiki shirika la kitaalamu na
kisayansi katika nyanja za Kilimo, Elimu, Maendeleo ya jamii na Ustawi
wa jamii{Tanzania Home Economics Association(TAHEA)}limesema liko tayari
kumsaidia mtu binafsi, familia na jamii ya Tanzania kwa ujumla kijamii
na kiuchumi kwa kutoa elimu ya fani mbalimbali.
Hayo
yamesemwa na mratibu wa shilrika hilo Bw Peter Mapunda, wakati alipokuwa
akizungumzia mipingo ya TAHEA, inayotekezwa kwa sasa ambao ni Mpango wa
kuhudumia watoto waishio katika Mazingira hatarishi.
Mipango
mingine ni Mradi wa kuhudumia watoto waishio katika Mazingira hatarishi
ngazi ya jamii katika wilaya ya Iringa kwa hisani ya watu wa Marekani
kupitia shirika la Africare pamoja na mpango wa Kujengea uwezo AZAKI
zinazotekeleza Mpango wa Pamoja Tuwalee wa kusaidia watoto waishio
katika Mazingira hatarishi ikishirikiana na shirika la Africare kwa
hisani ya watu wa Marekani mikoa ya Iringa Njombe, Dodoma na Singida
Aidha Bw
Mapunda amesema Katika huduma ya elimu ya chakula na lishe watoto 6418
kati yao wakike wakiwa 3105,walifikiwa kupitia walezi wao huku watoto
405 wakiume 205,na wakike 200 walisaidiwa chakula na watoto wengine
520,waliopo chini ya miaka mitano walihakikiwa kuangalia hali ya lishe.
Hata
hivyo mratibu huyo ameongeza kuwa kwa mwaka 2013 walihamasisha uundwaji
wa vikundi vya kuweka na kukopa na vile vya uzalishaji mali pampja na
kutoa elimu ya chakula na lishe.
(MM)
Comments