Dodoma. Wakati wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wakipitisha Rasimu ya
Kanuni za kuendesha Bunge hilo, suala la aina ya kura kwa ajili ya
kuamua masuala mbalimbali, limekwama na litaamuliwa na wabunge baada ya
kuanza kwa vikao rasmi vya Bunge hilo.
Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba,
Mchungaji Christopher Mtikila akimlalamikia Mwenyekiti wa muda wa Bunge
hilo kwa kutompa nafasi ya kuchangia bungeni mjini Dodoma jana. Picha na
Silvan Kiwale
Hatua hiyo imekuja baada ya kuwapo kwa mvutano wa takriban wiki nne kuhusu rasimu, hasa kifungu cha 37 na 38 kinachoeleza aina ya kura kati ya wazi na ya siri.
Hatua hiyo imekuja baada ya kuwapo kwa mvutano wa takriban wiki nne kuhusu rasimu, hasa kifungu cha 37 na 38 kinachoeleza aina ya kura kati ya wazi na ya siri.
Hata hivyo, wajumbe wawili wa Bunge hilo, Mchungaji Christopher Mtikila
wa DP na Felix Mkosamali wa NCCR- Mageuzi walisusia kupitisha azimio la
kukubali Kanuni za Bunge hilo, wakidai kusalitiwa katika uamuzi huo na
wenzao walioko kwenye Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Wajumbe na viongozi mbalimbali wa vyama vyenye ushawishi bungeni, kwa
pamoja waliridhia na kulegeza misimamo yao ili upatikane mwafaka wa
kutengeneza Katiba Mpya ndani ya wakati.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti ndani na nje ya Ukumbi wa Bunge mjini
Dodoma, viongozi hao walisema masilahi ya Watanzania katika mchakato wa
Katiba ni ya muhimu kuliko masilahi binafsi ya makundi.
Kinana asema
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Abdulrahaman Kinana alisema pamoja
na malumbano makali yanayoendelea katika Bunge la Katiba, anaamini sasa
Katiba itapatikana.
Comments