Katibu wa
Wabunge wa Tanzania Katika Bunge la Afrika Mashariki, Mhe. Shy-Rose
Bhanji (pichani) amerejea nchini baada ya ziara ya siku 10 ya Wabunge wa
EALA nchini Kenya. Hapa chini ni ujumbe wake kwa Serikali ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania.
Nimerejea
nchini baada ya ziara ya siku 10 nchini Kenya. Ziara hii ya wabunge wa
EALA ilikuwa kwa mwaliko wa Serikali ya Kenya lengo likiwa kuhamasisha
wananchi wa Kenya kupata ufahamu mkubwa juu ya Mtangamano wa Jumuiya na
faida zake. Tulipata nafasi ya kuonana na wananchi, wafanyabiashara,
wabunge, maseneta, magavana, asasi za kiraia na makundi mengine.
Ziara hii
imenifungua macho zaidi kwamba bado tuna kazi kubwa mbele yetu
kuhakikisha kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki inakuwa ni ya Wananchi
(people Centred Integration).
Kama
nilivojionea mwenyewe kwa upande wa maeneo mbalimbali tuliyoyafikia bado
mwamko wa ufahamu wa masuala ya EAC mdogo sana na kiu wa kuifahamu ni
kubwa.
Hata
hivyo Serikali ya Kenya kwa kuhakikisha wananchi wengi zaidi wanashiriki
kikamilifu juu ya masuala ya Jumuiya imefufua mpango huu wa wabunge wa
EALA kufika Kenya kuendelea na zoezi la uhamasishaji.
Ni imani
yangu kwamba na Serikali ya Tanzania itaiga mfano huu mzuri wa kuwaalika
wabunge wa EALA kufika nchini ili kuwafikia makundi mbalimbali hapa
nchini kwa lengo la kuhamasisha. Hata kwa upande wa Tz bado ufahamu wa
wananchi wengi zaidi juu ya masuala ya Integration ni changamoto kubwa.
Lengo kuu
la uanzishwaji wa EAC ni kuinua hali ya kiuchumi kwa wananchi wa EA
ambao sasa ni takriban millioni 140. Na iwapo mwamko wa wananchi ni
mdogo basi lengo hili litachukua muda mrefu sana kufikiwa au
kutokufikiwa kabisa. (FM) .Source http:.mjengwablog.com
Comments