Skip to main content

WABUNGE DODOMA WAWAPONDA BONGO MOVIE..WASEMA NI OMBA OMBA


SKENDO nzito ya Bongo Muvi imeibuliwa na baadhi ya wabunge waliopo mjini Dodoma kufuatia kuwalipua wasanii wake kuwa, ni ombaomba balaaKwa mujibu wa wabunge hao ambao walitaka majina yao yasitiriwe kwa sasa, baadhi ya wasanii hao ambao wengi ni mastaa wamekuwa wakiwazukia na kuwapiga mizinga jambo linalowashangaza hasa wakizingatia kuwa, wapiga mizinga hao wana majina makubwa na huonekana wakitembelea magari ya kifahari.
Staa wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper.
“Hivi nyie mapaparazi, mnashindwa kabisa kukomesha hii tabia ya mastaa wa Bongo Muvi? Hawa jamaa ni ombaomba sana.
“Wamekuwa wakitupiga mizinga sana. Tunawashangaa maana wengine wana majina makubwa, wanatembelea magari ya kifahari lakini bado wanaomba pesa ndogo,” alisema mbunge mmoja ambaye anatoka kwenye moja ya majimbo ya Mkoa wa Dar es Salaam.

KINACHOWASHANGAZA WABUNGE

Kwa mujibu wa wabunge hao, linalowashangaza zaidi ni kwamba wasanii hao ambao  ni wake kwa waume, wamekuwa wakipiga mizinga ya pesa ndogo badala ya kuomba pesa za kufanyia mambo makubwa yenye mikakati mizito.
Steve Mangere ‘Steve Nyerere’.
“Mtu anakuja, anasema anasumbuliwa na kodi ya nyumba au anasema hajala. Hivi kweli mastaa wakubwa kama akina…(anataja jina) ni wa kuomba vijisenti kama vya kodi ya nyumba jamani?” alihoji mbunge mwingine kati ya watano waliokuwa wakizungumza na gazeti hili.
Waheshimiwa hao waliendelea kuwaanika mastaa hao kwa kudai kwamba, walichogundua ni kuwa inapotokea wakapewa hitaji lao la fedha, huishia kukaa baa hadi usiku wa manane na asubuhi wakiamka wako vilevile kama hawakupewa.

MWAKIFWAMBA ABANWA NA RISASI

Ili kuweka sawa madai hayo mazito na yenye aibu kubwa kwa tasnia hiyo maarufu nchini, Risasi Jumamosi lilimtafuta Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania ‘TAFF’, Simon Mwakifwamba ambaye alikiri kuwepo kwa malalamiko hayo ya wasanii wake kuwa ombaomba!

HUYU HAPA MWAKIFWAMBA

“Ni kweli kabisa. Mimi mwenyewe nimewahi kusikia malalamiko hayo, lakini unajua tena ni mambo binafsi, mtu anapiga mizinga kwa mambo binafsi si rahisi kumwingilia,” alisema rais huyo.
Aliendelea kusema kuwa, katika vikao mbalimbali vya kisanii, amewahi kuweka wazi msimamo wa taasisi kwamba kila msanii aishi maisha yenye heshima huku akiwa mbali na mazingira yenye kusababisha aibu katika jamii.

KUMBE HATA JK ALIWAHI KUMLALAMIKIA

Katika kuonesha hasira zake juu ya tuhuma hizo zenye dharau katika gemu la filamu, Mwakifwamba alikwenda mbele zaidi kwa kusema kuwa, katika moja ya mazungumzo yake na Rais wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Kikwete ‘JK’ aliwahi kumlalamikia kwamba, wapo mastaa ambao kazi yao ni kupiga mizinga isiyo na tija.
“Rais mwenyewe aliwahi kuniambia kuna wasanii wakiwasiliana na yeye wanamwambia mambo ya pesa za kula.
“Kuna msanii aliwahi kumtumia meseji JK akimwambia, ‘mjukuu wako leo hali mbaya’,” alisema Mwakifwamba.
Akaendelea: “Sasa we’ unakutana na rais badala ya kumweleza mikakati mikubwa na nini cha kusaidiwa kuifanya tasnia iweze kuendelea, unapiga mizinga hujala, ni aibu sana.”

WALISHAMPIGA ‘MIZINGA’ HADI ‘MTOTO WA MKULIMA’

Mwakifwamba hakukubali kufumba midomo yake bila kupasua yote ambapo alizidi kudai kuwa, hawashangai sana wasanii wake hao kwani waliwahi kumpiga mizinga hadi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda ‘Mtoto wa Mkulima’.
“Niliwahi kukutana na Waziri Mkuu Pinda, nikamwomba mambo ya kuisaidia tasnia ya filamu Tanzania, akasema afadhali mimi nimeongea vitu vya maana, kuna wenzangu alikutana nao ‘wakambomu’ fedha za matumizi binafsi, nilishangaa sana,” alisema Mwakifwamba.

RISASI LAWASAKA MASTAA, WAPATIKANA HAWA:

Jacqueline Wolper, ni staa wa filamu za Kibongo. Filamu yake ya kwanza ni Ama Zao Ama Zangu. Yeye alipoulizwa kuhusu madai hayo, alisema:
“Ni kweli, sikatai kwamba hiyo tabia ipo tena sana tu. Lakini wanaoongoza ni mastaa wa kiume, hao ndiyo wanaotutia aibu ya kuonekana sisi ni o
mbaomba.”

STEVE NYERERE

Yeye ndiye Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity. Alisema anavyojua kuna kuonana kirafiki na waheshimiwa na kuonana kiajenda.
“Tabia ya kuomba fedha kwa waheshimiwa ipo. Lakini linapokuja suala la tasnia yetu kupeleka hoja kwao, tunaanza hoja baada ya hapo kuna waheshimiwa wengi wana urafiki na wasanii, tunaitana pembeni na kupiga kirungu.
“Siwezi kukaa na waheshimiwa kama Rostam Aziz, William Ngeleja, Mheshimiwa Abood na Nimrod Mkono halafu nikawaacha hivihivi, kisa eti mimi ni Mwenyekiti wa Bongo Muvi,” alisema Steve akionesha kumshangaa mwandishi aliyempigia simu kutaka usawa wa mizani ya habari hiyo.
Jennifer Kyaka ‘Odama’.
ODAMA YEYE
Jennifer Kyaka ‘Odama’ yeye alipata umaarufu mkubwa kupitia Tamthiliya ya Odama iliyokuwa ikirushwa na Televisheni ya Taifa (wakati huo TVT). Alipopigiwa simu iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa licha ya kurudiwa mara kadhaa.
                                                                                 Aunt Ezekiel
AUNT EZEKIEL
Risasi pia lilimtafuta  nyota mwingine aliye mahiri kwenye sinema za Bongo, Aunt Ezekiel ambaye filamu iliyompaisha sana inaitwa Miss Tanzania. Yeye simu yake ya mkononi ilionesha kutokuwa hata na laini kwa wakati huo.
Staa mkongwe katika gemu, Vincent Kigosi ‘Ray’.
RAY AFUNGUKA
Staa mkongwe katika gemu tangu enzi za Kaole Sanaa Group, Vincent Kigosi ‘Ray’ aliposakwa na kuulizwa kuhusu madai hayo ya wasanii kuwa ombaomba alisema:
“Wasanii wengi wanawaza maisha ya hapa na si baadaye. Badala ya mtu kuweka shida zake kwenye mfuko wa karatasi, anaweka kwenye rambo ambao unapiga kelele.
“Mwisho wa siku anaomba shilingi milioni tatu akagombolee gari au asaidiwe kodi ya nyumba, anasahau kuwa kapata nafasi ya kuonana na mheshimiwa azungumzie tasnia tunavyonyonywa hadi kuuza hati miliki,” alisem Ray.

Comments

Popular posts from this blog

MBINU ZA KUMFIKISHA MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KILELENI KWA HARAKA

Kwa kawaida wanawake wanafikia kilele (mwisho wa utamu wa ngono) kati ya dakika ishirini na saa moja, yaani kwa kifupi inawachukua muda mrefu sana hali inayopelekea mpenzi mvivu kuchoka na ufanyaji wake utakuwa wa “ovyo” hali itakayo kufanya wewe kuishiwa na hamu ya kuendelea. Pamoja na kuchelewa huko ambako kunatokana na utofauti wetu kati ya mwanaume na mwanamke lakini nakumbuka hapo nyuma nilikutana na wanawake 2 waliokuwa ndani ya ndoa na wamezaa lakini hawajawahi kabisa kujua utamu wa tendo hilo alimaharufu kama “kufanya mapenzi”. Natambua kuwa ni ngumu au niseme si wanawake wote ambao wamejaaliwa kimaumbile kwamba wanafanikiwa kufika kileleni zaidi ya mara mbili kila wanapofanya mapenzi/ngono (kumbuka ni kati ya dakika 15 na saa moja hivyo Jibaba hapa awe na uwezo wa kujizuia kwa zaidi ya dk 45) na ikiwa jamaa ni “mzamiaji” basi unaweza ukaondoka na goli 3 ktk mzunguuko mmoja. Lakini kwa nini basi baadhi yao tu ndio wafike kileleni na wengine was...

Mushikiwabo to UN: Enhance civilian protection

By Eugene Kwibuka Rwanda’s Minister of Foreign Affairs and Cooperation has urged the United Nations Security Council (UNSC) to invest more energy in the prevention of conflicts for better protection of civilians living in conflict-torn areas. Rwanda’s Foreign minister, Louise Mushikiwabo Louise Mushikiwabo made the call during an open debate on the protection of civilians in armed conflict which the UNSC held in New York on Tuesday. “Rwanda’s core message today is that enhancing the protection of civilians in armed conflict requires action before a conflict starts. The proliferation of non-state armed groups makes civilian protection both more urgent, and harder to achieve,” she said. For better protection of civilians in armed-conflict areas, the minister emphasised the need to increase investments in professionalising the military and police forces through adequate training. “Only when the leadership of armed forces shares the international...

Saudi King urges U.N. action against religious insults

Saudi King Abdullah urged the United Nations to produce a resolution condemning insults on monotheistic religions after the anti-Islam film in the U.S. that sparked deadly protests in many Muslim countries last month. (AFP) By AFP, MINA/SAUDI ARABIA Saudi King Abdullah on Saturday demanded a U.N. resolution condemning insults on monotheistic religions after a low-budget film produced in the U.S. sparked deadly protests last month. “I demand a U.N. resolution that condemns any country or group that insults religions and prophets,” he said during a meeting at his palace with religious figures and heads of hajj delegations in the Mina valley where pilgrims were performing final rituals of hajj. “It is our duty and that of every Muslim to protect Islam and defend the prophets.” A low-budget film produced in the U.S., Innocence of Muslims, triggered a wave of deadly anti-American violence last month across the Muslim world targeting US symbols ranging ...