imekuwa ni dhana ya muda mrefu miongoni mwa wanajamii katika Afrika kuwa msichana hawezi kuolewa na mwanamume waliyelingana umri kwa kuwa ni vigumu kuelewana na kuheshimiana. Dhana hiyo inajikita katika kuchambua tofauti ya ufahamu kati ya mwanamke na mwanamume wenye umri sawa. Mwanamke huwa na akili iliyokomaa zaidi kuliko mwanamume wa umri huo huo. Utafiti mpya umeipa uzito nadharia yao, baada ya kugundua kuwa ubongo wa msichana hukomaa haraka kuliko wa mvulana
Watafiti kutoka Chuo Kikuu cha
Newcastle wamasema hii inaweza kusaidia kuelezea sababu za wasichana
wadogo kuonekana kukua kwa kasi zaidi, kuliko wenzao wa kiume wenye umri
sawa.
Wanasayansi walitumia kipimo maalumu
kwa ajili ya kuchunguza ubongo kwa watu 121 waliokuwa na umri kuanzia
miaka minne hadi 40. Matokeo ya utafiti huu yalionyesha kwamba mchakato
wa kubalehe huanza kati ya miaka 10 kwa msichana, huku mvulana huchukua
muda mrefu kuanzia miaka 11 mpaka 20.
Dk. Marcus Kaiser, ambaye nbi mtafiti, anasema: "Hii ni sehemu ya mchakato wa kawaida wa kujifunza ubongo kwa jumla.
"Msichana pia anawahi kupevuka
ukilinganisha na mvulana, lakini akishabalehe tu ubongo wake hukomaa
haraka na hapo ndipo maumbile yake yanapoanza kujitengeneza mapema kwa
ajili ya mwili kujitayarisha kubeba ujauzito wakati wowote. Hata hivyo
akili yake hukua kwa nafasi kubwa kipindi hiki, ukilinganisha na
mwanamume ambaye ni hadi miaka 10 baadaye," anasema Edwin.
Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi katika
Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, Dk. Elifatio Towo anasema mtoto
yeyote ana uwezo wa kukua kwa haraka zaidi, kutokana na namna mzazi
anavyomlisha na haina tofauti na jinsi yake.
"Ikumbukwe kwamba mtoto yeyote anaweza kukua kwa haraka zaidi ikiwa mzazi atampa lishe bora na matunzo mazuri.
Kunyonyesha ndiyo sababu pekee
inayowafanya watoto akili zao zikue kwa haraka zaidi. Lakini ikumbukwe
kwamba watoto wa kike huwa na busara zaidi katika baadhi ya mambo na
katika kufanya uamuzi ikilinganishwa na wa kiume," anasema na kuongeza:
"Huyu anaweza kufikiria makubwa zaidi
ya umri alionao, lakini mara nyingi inatokana na maumbile kwamba yeye ni
mwanamke hivyo kupevuka na anakuwa tayari kubeba ujauzito, mwili wake
unajitengeneza wenyewe," anasema Dk. Towo.
Wasemavyo wazazi
Maimuna Jitegemee, mama mwenye watoto
watatu, anasema "Binti yangu niliweza kumwachia nyumba akiwa na umri wa
miaka 13 tu, niliweza kusafiri na kurudi. Hata hivyo hali imekuwa
tofauti kwa mtoto wangu wa kiume, kwani licha ya kwamba dada yake yupo
chuoni hivi sasa, siwezi kumwachia nyumba japokuwa ana umri wa miaka 15.(E.L)Source:www.mjengwablog.com
Comments