LIGI SOKA DARAJA LA KWANZA TZ BARA TOTO YAINYUKA 2-0 POLISI MARA
Ma-Kapteni
wa timu za Toto (kulia) na Polisi Mara (kushoto) wakisalimiana mbele ya
waamuzi kabla ya mchezo wao wa Ligi Soka Daraja la Kwanza Tanzania
Bara, uliochezwa uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, dakika 90
zikimalizika Toto 2, Polisi Mara 0.
Kikosi cha Polisi Mara kilichoshuka leo dimbani CCM Kirumba kukabiliana na Toto Africans.
Mchezo wa Ligi soka daraja la Kwanza Tanzania bara katika kundi C
baina ya Toto Africans na Polisi Mara umemalizika dimbani CCM Kirumba
jioni ya leo kwa Toto Africans ya jijini humo kuibuka na ushindi mnono
nyumbani kwa kuwabugiza Maafande wa Mara, bao mbili sifuri (2-0).Inatoka kwa mdau.
Comments