Uongozi
wa Klabu ya Simba umeweka wazi kuwa suala la kumuongezea mkataba kocha
wake mkuu wa sasa, Zdravko Logarusic limewekwa pembeni kwa kuwa
wanasubiri kuona mwelekeo wa timu yao ambayo imekuwa haina matokeo
mazuri hivi karibuni.
Loga raia wa Croatia alisaini mkataba wa miezi
sita wakati alipotua klabuni hapo mwishoni mwa mwaka jana, ambapo
mkataba huo unatarajiwa kufikia tamati Juni mosi, mwaka huu.
Katibu
Mkuu wa Simba, Ezekiel Kamwaga, aliweka wazi kuwa matokeo ya timu
katika mechi zilizosalia ndiyo yatapa picha uongozi juu ya kuongeza au
kutoongeza mkataba huo.
“Mkataba
wake unatarajiwa kufikia tamati Juni mosi, mwaka huu tutaendelea naye
mpaka mwisho wa ligi, makubaliano yetu ya awali yalikuwa ni kumpa
mkataba wa muda mfupi ili kumuangalia na iwapo atafanya vizuri na
kuridhisha basi tutamuongezea.
“Lakini
suala hilo litaamuliwa mwisho wa ligi kwa wanachama na viongozi
kutathmini kile alichokifanya na kama kubaki ama kutobaki ni maamuzi
yatakayotolewa hapo baadaye,” alisema Kamwaga.
Simba
inashika nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu Bara ambapo hivi
karibuni iliambulia pointi mbili kati ya 12 ilizotakiwa kuzipata katika
mechi nne za ligi hiyo.Inatoka kwa mdau.
Comments