Mcheza sinema maarufu Lupita Nyong’o ambaye ni raia wa Kenya, Jumapili
ameshinda tuzo la kifahari la Oscar huko Hollywood California.
Lupita Nyong'o,ameshinda tuzo ya muigizaji
bora msaidizi katika filam aliyoshiriki "12 Years a Slave", akizungumza
katika tuzo za 86 za Oscar huko Hollywood, California March 2, 2014.
REUTERS/Lucy Nicholson (UNITED STATES TAGS: ENTERTAINMENT) (OSCARS-SHOW)
- RTR3FY5W
Lupita alipata tuzo hilo kwa kuwa muigizaji msaidizi bora zaidi kwenye filamu iitwayo“12 years A Slave”.
Baada ya kupokea tuzo hilo, Lupita alitoa hotuba yenye hisia kali na
kuwashukuru wote waliomwezesha kushinda tuzo hilo la Oscar.
Awali macho ya dunia kwa wapenzi wa filam yalielekezwa huko Hollywood
kutizama tuzo za mwaka wa 86 za Oscar zikitunukiwa wasanii mbali
mbali wa filam duniani.
Kwa upande wa Afrika mcheza filamu mwingine wa mara ya kwanza Barkhad
Abdi ambaye ni raia wa Somalia aliteuliwa kuwania katika nafasi ya
waigizaji wasaidizi ambapo alishiriki katika filamu “Captain Phillips”
ambapo muigizaji Jared Leto alipata ushindi.
Vyombo vya habari vya Kenya viliripoti kuwa wakenya na waafrika kwa
jumla walikuwa wakisubiri kuona ikiwa muigizaji Lupita Nyong’o atapata
tuzo hilo. Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pia alikuwa ametuma salamu za
kumtakia ushindi Lupita ,katika ujumbe kwenye ukurasa wake wa
Facebook.
Via voa
Comments