Skip to main content

Posts

Showing posts from March, 2014

Muungano Day Celebration – 50 Years April 1964 - April 2014

On Saturday, April 26, 2014, Tanzania will celebrate Muungano (Union) Day. It is a public holiday in Tanzania, commemorating the day Zanzibar and Tanganyika joined together to form The United Republic of Tanzania. After The United Republic of Tanzania was formed in 1964, the late Mwalimu Julius Kambarage Nyerere became the first President of the new Republic, and the late Sheikh Abeid Karume, then the President of Zanzibar, became the First Vice President and Chairman of the Revolutionary Council. The late Rashidi Mfaume Kawawa became the Second Vice President in charge of Government business in the National Assembly. The history of the union of Tanganyika and Zanzibar is undoubtedly unique. These two States agreed to unite for the benefit of all Tanzanians. INVITATION TO ALL The Tanzanian Ambassador to the United States of America, H.E. Liberata Mulamula, invites you all to the 50th Anniversary of the United Republic of Tanzania, Muungano day 2014. The ...

Obama lands in Saudi Arabia for talks on U.S role in Mideast

By Reuters Saudi Arabia concerned U.S. losing interest in region; U.S. president reassures Saudi king U.S. will not agree bad deal with Iran. U.S. President Barack Obama reviews an honor guard upon his arrival in Riyadh, Saudi Arabia March 28, 2014. Photo by Reuters U.S. President Barack Obama and Saudi King Abdullah discussed "tactical differences" in their approach to some issues during a meeting in Riyadh on Friday, but agreed both sides remain strategically aligned, a senior U.S. official said. Obama also assured Abdullah that the United States would not accept a bad nuclear deal with Iran. In the runup to his visit to the kingdom, officials had said Obama would aim to persuade the monarch that Saudi concerns that Washington was slowly disengaging from the Middle East and no longer listening to its old ally were unfounded. Last year senior Saudi officials warned of a "major shift" away from Washington after bitter disagreem...

Nyota wa anga za filamu Nigeria akana kuvunjika Ndoa na mkewe

LAGOS, Nigeria KATIKA siku za hivi karibuni, kumekuwepo na uvumi kwamba, mwigizaji Emeka Ike na mkewe, wamekuwa katika msuguano mkali uliosababisha watengane. Kwa mujibu wa habari hizo, mke wa Emeka alidai talaka kutoka kwa mumewe kutokana na kuchoshwa na tabia za mwigizaji huyo. Habari hizo ziliendelea kueleza kuwa, kutokana na ndoa ya wawili hao kuvunjika, Emeka aliamua kuwachukua watoto wao wawili na kwenda nao Abuja, akimuacha mkewe akibaki na watoto wengine wawili mjini Lagos. Hata hivyo, Emeka amekanusha vikali habari hizo na kuziita kuwa ni za uzushi. Emeka ameandika kwenye mtandao wa facebook wiki hii: " Huu ni uzushi." Mbali na kuandika maneno hayo, Emeka aliweka picha aliyopiga pamoja na mkewe na watoto wao wanne.

Msome Okwi kuhusu Mbeya City

Na Emmanuel Ndege MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Yanga, Emmanuel Okwi, amesema anakunwa na kiwango cha juu cha soka kinachoonyeshwa na timu ya Mbeya City katika michuano ya ligi kuu ya Tanzania Bara. Akizungumza na Burudani makao makuu ya klabu hiyo, mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam juzi, Okwi alisema Mbeya City imeleta changamoto mpya katika ligi kuu msimu huu. Okwi alisema timu hiyo yenye makao makuu yake mjini Mbeya, haijayumba kisoka tangu ligi kuu ilipoanza na wachezaji wake wanacheza kwa kujiamini na bila kukata tamaa. "Iwapo wataendelea hivi msimu ujao, haitakuwa ajabu kwa Mbeya City kutwaa ubingwa,"alisema mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uganda. Okwi amekiri kuwa, ligi ya msimu huu ni ngumu na yenye ushindani mkali na hakuna timu yenye uwezo wa kutangaza ubingwa mapema. "Nimeichezea Simba kwa miaka zaidi ya miwili. Huko nyuma timu zilikuwa na uwezo wa kutangaza ubingwa zikiwa zimesalia mechi mbili au tatu, lakini msimu huu ni ...

NEWS EMBARGO:Not for Publication or Distribution before 31March 2014

PRESS RELEASE “The food security project for underprivileged farmers” On 31 th March , 201 4 , the Government of Japan and the Government of the United Republic of Tanzania will sign Exchange of Notes for the Japan eseGrant Project “The food security project for underprivileged farmers ”. The g rant which will be provided from the Government of Japan, amounts to three hundred and eighty m illion Japanese Yen ( \ 380,000,000), approximately six billion ninety million Tanzanian Shillings (Tsh6,061,000,000). This project aims to improve food production, especially for underprivileged farmers, and its ultimate goal is to enhance food security in Tanzania. The grant is provided to the Government of Tanzania for procurement of fertilizer. After the procurement, the fertilizer will be supplied to farmers through private companies. The income derived from the sale of the fertilizer can make it possible for the Government of Tanzania to support agricultural dev...

UCHAGUZI CBE MWANZA 2014 NI ZAIDI YA URAIS

Huu ni msafara wa mmoja kati ya wagombea uchaguzi wa Rais wa Serikali ya wanafunzi Chuo cha Biashara CBE Mwanza.  Hapatoshi. Mazingira ya Chuo. Kama kuna viashiria fulani hivi... au macho yangu? Wagombea Mashariki. Wagombea Magharibi. MATOKEO TUTAYAANIKA HAPA HAPA,Source G Sengo

Serikali ya Somalia, ASWJ walumbana juu ya ujumuishwaji wa wanamgambo kwenye SNA

Na Hamdi Salad, Mogadishu Serikali ya Somalia inakabiliwa na upinzani kutoka Ahlu Suna wal Jamaa (ASWJ) baada ya pande hizo mbili kutokufikia makubaliano juu ya kuviunganisha vikosi vyao kwenye kampeni ya kijeshi inayoendelea sasa dhidi ya al-Shabaab mkoani Galgadud. Wanajeshi wa Jeshi la Taifa la Somalia (SNA) wakiwa wamekaa kwenye lori mjini Qoryooley baada ya operesheni iliyofanikiwa kwenye Kikosi cha Umoja wa Afrika nchini Somalia kuukomboa mji huo kutoka kwa wanamgambo wa al-Shabaab siku ya tarehe 22 Machi 2014. [PICHA YA AFP / AU UN IST / TOBIN JONES] Uhusiano kati ya serikali na wanamgambo hao wanaoshirikiana na serikali yalianza kuzorota mwishoni mwa mwaka jana juu ya ahadi ambazo hazikutekelezwa, naibu mwenyekiti wa kamati tendaji ya ASWJ, Sheikh Ahmed Abdullahi Ilkaase, aliiambia Sabahi. Wakati operesheni ya jeshi la serikali ilipokaribia kwenye maeneo yanayodhibitiwa na ASWJ, serikali ilituma ujumbe mjini Dhusamareb, mji mkuu wa mkoa wa...

Warioba:‘Tumemaliza kazi yetu’

Na Editha Majura, Mwananchi Dodoma. Siku moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kuzindua Bunge na kuponda ripoti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Joseph Warioba amesema jukumu walilopewa kwa mujibu wa sheria wamelikamilisha na wanawaachia wananchi waamue. Jaji Joseph Warioba Akizungumza na Mwananchi jana asubuhi, Jaji Warioba alisema alichokizungumza Rais Kikwete ni maoni yake na kwamba hawezi kuyajadili. “Rais Kikwete alichozungumza ni maoni yake, kwa sasa sipendi kuyazungumzia hayo, ” Jaji Warioba alieleza. Alisema wamemaliza jukumu walilopewa na kwamba sasa jukumu lote lipo mikononi mwa Bunge. Jaji Warioba alisema Tume yake ilikusanya maoni kutoka kwa wananchi, mabaraza ya wilaya ya Katiba na Taasisi mbalimbali, wakatengeneza rasimu ambayo sasa wameikabidhi kwa Bunge Maalumu la Katiba. Jaji Warioba pia alikataa kuzungumzia zogo lililoibuka bungeni na kusababisha rasimu kuwasilishwa Jumatano, baada ya kikao cha Juman...

TAHEA wajitolea kusaidia watoto Katika huduma ya elimu ya chakula na lishe

Na Martha Magessa Ili kusaidia jamii kuondokana na adui umasiki shirika la kitaalamu na kisayansi katika nyanja za Kilimo, Elimu, Maendeleo ya jamii na Ustawi wa jamii{Tanzania Home Economics Association(TAHEA)}limesema liko tayari kumsaidia mtu binafsi, familia na jamii ya Tanzania kwa ujumla kijamii na kiuchumi kwa kutoa elimu ya fani mbalimbali. Hayo yamesemwa na mratibu wa shilrika hilo Bw Peter Mapunda, wakati alipokuwa akizungumzia mipingo ya TAHEA, inayotekezwa kwa sasa ambao ni Mpango wa kuhudumia watoto waishio katika Mazingira hatarishi. Mipango mingine ni Mradi wa kuhudumia watoto waishio katika Mazingira hatarishi ngazi ya jamii katika wilaya ya Iringa kwa hisani ya watu wa Marekani kupitia shirika la Africare pamoja na mpango wa Kujengea uwezo AZAKI zinazotekeleza Mpango wa Pamoja Tuwalee wa kusaidia watoto waishio katika Mazingira hatarishi ikishirikiana na shirika la Africare kwa hisani ya watu wa Marek...

Kim Kardashian wears wedding dress as she FINALLY lands first American Vogue cover... with fiancé Kanye West

Cover stars: Kim Kardashian and Kanye West have finally made the front cover of U.S. Vogue, appearing on the front of the April edition  Adorable: An accompanying video on the website shows Kim, Kanye and baby North  Daddy's girl: Kanye plants a kiss on his bouncing baby's head while sitting on a plane in the video Outdoor shoot: The video went behind the scenes of the prestigious photo session Living the high life: Kim and Kanye's jet setting adventures are explored in the photographs Living the high life: Kim and Kanye's jet setting adventures are explored in the photographs  In love: The video is set to Kanye's controversial video Bound 2 in which Kim appears in the video  Dramatic scenes: In one snapshot, Kim sports a ruffled white dress, laying back against a car, while Kanye stands in front of her  Behind the scenes: The famous twosome looked happy and relaxed for their big shoot  ...

Washiriki shindano la Maisha Plus waingia kijijini rasmi

Uzinduzi wa Kijiji cha Maisha Plus; Jana washiriki wapatao 29 waliingia katika kijiji cha Maisha Plus kuanza kukabiliana na changamoto za maisha kuwania shilingi milioni 25 za Kitanzania. Pichani ni Mkuu wa Kijiji...Mwite babu wa kaya akiwepo kuhakikisha wanakijiji wanakaribishwa kwa shangwe kijijini hapo. Ofisa Mtendaji wa Kampuni ya dMb ambao ni wamiliki wa Maisha Plus, Masoud Ally (Masoud kipanya kulia) akizungumza katika uzinduzi wa Kijiji cha Maisha Plus, ambapo jana washiriki wapatao 29 waliingia kijijini kuanza kukabiliana na changamoto za maisha kuwania shilingi milioni 25 za Kitanzania. Mmoja ya wawakilishi toka Oxfam ambao ni wadhamnini wa Maisha Plus 2014 akizungumza machache. Pembeni yake ni Afisa mtendaji wa Kampuni ya DMB ambao ni wamiliki wa Maisha Plus Masoud Ally (Masoud kipanya). Safari ya kuelekea kijiji cha...

MADADI MKURUGENZI MPYA WA UFUNDI TFF

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemteua Salum Madadi kuwa Mkurugenzi wake mpya wa Ufundi. Uteuzi huo umefanya na Kamati ya Utendaji katika kikao chake cha dharura kilichofanyika jana (Machi 19 mwaka huu) jijini Dar es Salaam. Kabla ya uteuzi, Madadi alikuwa akikaimu nafasi hiyo tangu Januari mwaka huu baada ya Mkurugenzi wa Ufundi aliyekuwepo kumaliza mkataba wake Desemba 31 mwaka jana. Madadi mwenye leseni A ya ukocha ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) ni kocha mwenye uzoezi wa zaidi ya miaka 30 ambapo alianza kufundisha mpira wa miguu mwaka 1980 katika klabu ya Maji SC ya Lindi. Ana elimu ya sekondari aliyoipata katika shule ya Chidya na diploma ya ukocha wa mpira wa miguu aliyoipata nchini Ujerumani. Pia ni Mkufunzi wa makocha wa CAF, na alijiunga na TFF mwaka 2006 akiwa Ofisa Maendeleo. Alikuwa Kocha wa Taifa Stars mwaka 2000. Mbali ya Maji SC, amewahi kufundisha timu za Nyota Nyekundu, Ushirika ya Moshi, Simba, Shangani ya Zanzibar, ...

SOMA JINSI NYOTA WA ARSENAL TESEKA KATIKA UHUSIANO WA Celia Kay

MWANAMITINDO AMPASUA KICHWA  LONDON, England HATIMAYE mshambuliaji, Olivier Giroud wa klabu ya Arsenal ameamua kuvunja ukimya kwa kujibu tuhuma za kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamitindo, Celia Kay. Giroud anatuhumiwa kumpeleka Kay kwenye hoteli ya Four Seasons iliyoko Canary Wharf siku moja kabla ya Arsenal kuichapa Crystal Palace katika mechi ya ligi kuu ya England iliyochezwa Februari 2 mwaka huu. Kocha Mkuu wa Arsenal, Arsene Wenger, hadi sasa hajaamua kuweka wazi kuhusu hatua zitakazochukuliwa kwa Giroud baada ya kukiri kufanya mapenzi na binti huyo wakati akiwa katika majukumu ya kuitumikia timu yake. Wenger alikaririwa hivi karibuni akisema kuwa, suala la mchezaji huyo ni la ndani na litashughulikiwa na uongozi wa klabu. "Hili ni suala la ndani, sitaki kulizungumza hadharani kwa sababu naheshimu maisha yake binafsi,"alisema Wenger. Kay alimpiga picha Giroud alipokuwa kwenye chumba cha hoteli hiyo, akiwa amevaa chupi ya ndani na kuis...

KATIKA INSTAGRAM: WEMA SEPETU AWEKA PICHA HII YA DIAMOND NA KUANDIKA MANENO HAYA.

wemasepetu Da love of my life.... Dats wat he is.... Our life, our rules.... Sipendi watu wanavyoingilia my love life kabisa.... I am his nd he is mine... dats jus it.... Kama ni mshenzi ndo wangu, tahira wangu, hafai ndo tayari wangu.... Love him jus like dat.... Mapenzi huwa hayaingiliwi hata siku moja.... Nd dey say wapenzi wakigombana chukua jembe ukalime, hawakukosea at all... With all due respect stop talking shit bout my baby.... Cuz at da end of da day he is da one I love nd I aint scared to.say it.... Nd I aint gon.stop... Call me stupid, crazy or whatever but dats jus reality.... Take it or leave it.... Im out...

Mwanamke hupevuka kiakili mapema kuliko mwanaume

imekuwa ni dhana ya muda mrefu miongoni mwa wanajamii katika Afrika kuwa msichana hawezi kuolewa na mwanamume waliyelingana umri kwa kuwa ni vigumu kuelewana na kuheshimiana. Dhana hiyo inajikita katika kuchambua tofauti ya ufahamu kati ya mwanamke na mwanamume wenye umri sawa. Mwanamke huwa na akili iliyokomaa zaidi kuliko mwanamume wa umri huo huo. Utafiti mpya umeipa uzito nadharia yao, baada ya kugundua kuwa ubongo wa msichana hukomaa haraka kuliko wa mvulana Watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Newcastle wamasema hii inaweza kusaidia kuelezea sababu za wasichana wadogo kuonekana kukua kwa kasi zaidi, kuliko wenzao wa kiume wenye umri sawa. Wanasayansi walitumia kipimo maalumu kwa ajili ya kuchunguza ubongo kwa watu 121 waliokuwa na umri kuanzia miaka minne hadi 40. Matokeo ya utafiti huu yalionyesha kwamba mchakato wa kubalehe huanza kati ya miaka 10 kwa msichana, huku mvulana huchukua muda mrefu kuanzia miaka 11 mpaka 20. D...

WATAKAOVUNJA VITI UWANJA WA TAIFA KUKIONA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) tunalaani vikali fujo na uhabirifu wa mali unaofanywa na washabiki viwanjani wakati mechi mbalimbali zikiwemo zile za kimataifa na ligi za hapa nchini. Tunaiomba radhi Serikali kwa uharibifu wa viti uliotokea kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga ya Tanzania na Al Ahly ya Misri iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Uharibifu huo wa viti umesababisha hasara ya sh. milioni 15 kwa wamiliki wa uwanja huo ambao ni Serikali. TFF tutalipa fedha hizo kwa Serikali kutokana na uharibifu huo. Tunaendelea kuchunguza tukio hilo, huku tukijiandaa kutoa adhabu kwa klabu na washabiki husika kulingana na kanuni zetu. Adhabu itakuwa kali ili iwe fundisho kwa wengine. Kwa mujibu wa Serikali, viti kumi viling’olewa na kutupwa ovyo ovyo uwanjani wakati vingine 40 viliathirika kutokana na vurugu za watazamaji hao. Tumebeba dhamana ya kulipa uharibifu huo kwa vile TFF ndiyo wenye dhamana ya kusimamia mechi za kimatai...

VURUGU ZANZIBAR...!

Taarifa za mitandaoni , huko Zanzibar kumetokea vurugu,kupiga mawe magari ya serikali huku wafanyakazi wa serikali wakijeruhiwa .. Picha hapo juu inaonesha gari la Katibu mkuu wizara ya fedha na uchumi mheshimiwa Khamis Musa likiwa limepinduliwa, katika gari hakuwemo katibu hyuo mkuu bali  alikuemo dereva wake ambae mpaka sasa hali yake inaendelea vizuri, Tutaendelea kuwapa taarifa zaidi Chanzo:mitandao ya kijamii

Majengo yaporomoka York New

  Majengo mawili yameporomoka New York Marekani ambapo   imetoka ripoti ya watu wawili kufariki na wengine kutoonekana huku 18 wakijeruhiwa na wanne wakikimbizwa hospitali.   Chanzo cha majengo hayo kuporomoka ni mlipuko uliotokana na kuvuja kwa gesi ambapo askari wa zimamoto wakiwa na vifaa vya kisasa wako kwenye eneo la tukio kuendelea kuzima moto.

Jumba la Kifahari la Justine Bierber Balaa kubwa!!

Star wa reality TV Khloe Kardashian ameonekana katika jumba la kifahari la msanii Justine Bierber huko calabasas,califonia. Habari za uhakika zimesema kwamba mwanadada huyo ameinunua nyumba hiyo baada ya kuwekwa mnadani na idara ya polisi ya eneo hilo tangu mwaka jana mwishoni kwa sababu ambazo zimeelezwa kuwa Justine Bierber kushindwa kuishi vizuri na jirani zake ikiwemo kuwasababishia majirani zake hasara ya dola za kimarekani $20 000 sawa na shilingi mil 32 za kibongo Hakimu wa mahakama ya Los Angeles kwa sasa anapitia ushahidi wa yote yaliyotokea na baadae ataamua endapo atamfungulia mashtaka Justine Bierber.Meya wa Calabasas Fred Gaines amesema usalama wa makazi ya watu ni kitu cha muhimu zaidi kwao na kwa bahati mbaya wamekuwa na matukio mengi ya uvunjifu wa amani yanayomhusu Justine bierber na makosa hayo yameelezwa   wazi na idara ya polisi ya eneo hilo Justine(20) kwa sasa amepanga nyumba Atlanta,Georgia akiwa na mpango kwa kununua nyumba hiyo n...

Taarifa: Pingamizi dhidi ya mgombea wa CHADEMA kwenye Ubunge Chalinze

TAARIFA YA PINGAMIZI LA MGOMBEA WA UBUNGE JIMBO LA CHALINZE FABIAN LEONARD SKAUKI – MGOMBEA CHAMA CHA WANANCHI – CUF DHIDI YA MATHAYO MANG’UNDA TORONGEY – MGOMBEA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO - CHADEMA 13.03.2014 Mimi FABIAN L. SKAUKI, mgombea ubunge wa uchaguzi mdogo jimbo la CHALINZE kwa Ticket ya THE CIVIC UNITED FRONT (CUF) ninamwekea Pingamizi mgombea wa chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwamba amepoteza sifa za kuwa mgombea kwa sababu zifuatazo. Ndugu MATHAYO. M. TORONGEY amejaza Taarifa za uongo kwenye Fomu yake kwamba kazi anayoifanya ni BIASHARA. Sio kweli, kwa sababu hajaweka vielelezo vya yeye kufanya hiyo kazi. Hajulikani anafanya kazi gani. Ndugu MATHAYO .M. TORONGEY amejaza katika fomu kwamba anajua kusoma na kuandika Kiswahili na kiingereza. Taarifa hizi ni za uongo, mgombea huyu hajui kusoma wala kuandika Kiswahili wala kiingereza, na kwamba amedanganya na amepoteza sifa za kuwa mgombea. Ndugu MATHAYO .M.TO...

TIL This Week 21- Lupitaaa! Sexy Bacon Apps, Boosie back! Yayy??

by Houston Williams (@AllHipHopcom)     The latest episode of Amanda Seale’s Things I Learned (TIL) This Week delves deep. It dives so deep, it questions the release of Lil Boosie…(who would dare!?) Also, there is a deep, comedic and philosophical analysis of Lupita. Last but not least, Bacon Apps? Oh, you will have to see this non-cypher sh*t for yourself! Source all hip hop .com

Kura bado kitendawili Bunge la Katiba

Dodoma. Wakati wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wakipitisha Rasimu ya Kanuni za kuendesha Bunge hilo, suala la aina ya kura kwa ajili ya kuamua masuala mbalimbali, limekwama na litaamuliwa na wabunge baada ya kuanza kwa vikao rasmi vya Bunge hilo. Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Mchungaji Christopher Mtikila akimlalamikia Mwenyekiti wa muda wa Bunge hilo kwa kutompa nafasi ya kuchangia bungeni mjini Dodoma jana. Picha na Silvan Kiwale Hatua hiyo imekuja baada ya kuwapo kwa mvutano wa takriban wiki nne kuhusu rasimu, hasa kifungu cha 37 na 38 kinachoeleza aina ya kura kati ya wazi na ya siri. Hata hivyo, wajumbe wawili wa Bunge hilo, Mchungaji Christopher Mtikila wa DP na Felix Mkosamali wa NCCR- Mageuzi walisusia kupitisha azimio la kukubali Kanuni za Bunge hilo, wakidai kusalitiwa katika uamuzi huo na wenzao walioko kwenye Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa). Wajumbe na viongozi mbalimbali wa vyama vyenye ushawishi bungeni, kwa pamoja waliridhi...

Waandishi wa habari wazuiwa

Dodoma. Bunge Maalumu la Katiba limepitisha kanuni ya kuwazuia waandishi wa habari kuingia katika vikao vya kamati za chombo hicho, hatua ambayo inaelezwa ni kinyume na Katiba inayotoa uhuru wa wananchi kupata habari. Mwenyekiti wa muda wa Bunge la katiba,Pandu kificho.PICHA|MAKTABA Kanuni hiyo ilipitishwa jana baada ya malumbano makali yaliyowagawa wajumbe wa bunge hilo, baadhi wakipinga kifungu hicho kwa sababu kinavunja Katiba ya nchi inayotoa uhuru kwa waandishi kukusanya na kusambaza habari na wengine wakiunga mkono kuwazuia. Kanuni hiyo ilipitishwa kwa mbinde huku baadhi ya wajumbe wakiendelea kushikilia msimamo wa kuikataa, hata baada ya Mwenyekiti wa Muda wa bunge hilo, Pandu Ameir Kificho kuridhia kipite. Wajumbe waliopinga kanuni hiyo ni Joshua Nasari, Moses Machali, Peter Serukamba, Ezekiah Wenje na Maria Sarungi. Baadhi ya wajumbe akiwamo Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mukajanga walisimama kutaka kuzungumza lakin...

Watanzania wataka nchi ikumbukwe duniani

Washington. Ujumbe wa Tanzania katika mikutano muhimu inayofanyika Marekani wameipigia debe nchi yao wakitaka ikumbukwe. Katika mkutano wa 45 wa Kamisheni ya Takwimu ya Umoja wa Mataifa (UN) na mkutano wa wazi wa tisa wa kikosi kazi kuhusu mapendekezo ya ajenda za malengo mpya ya maendeleo endelevu baada ya 2015 (SDGs), wamekuwa wakitetea masilahi ya nchi kwa kushiriki na kuchangia majadiliano ya mada mbalimbali zinazohusiana na mikutano hiyo . Akichangia katika mada iliyohusu Technolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT), Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dk. Albina Chuwa alisema mwaka hadi mwaka Tanzania na Afrika imeendelea kupiga hatua katika teknolojia ya habari na mawasiliano licha ya changamoto mbalimbali. Alizitaja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni kutokuwapo kwa uratibu kati ya wazalishaji wa takwimu za ICT na watumiaji na kati ya wazalishaji na watoaji wa takwimu ambao ni chanzo muhimu cha taarif...