Mchungaji Josephat Gwajima Siku chache baada ya picha za mtoto mchanga kusambazwa katika mitandao ya kijamii na kudai kuwa ni za mtoto wa mwimbaji wa nyimbo za Injili nchini, Flora Mbasha kuwa amezaa na Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima hatimaye wawili hao wamefunguka. Hatua hiyo imekuja miezi saba tangu wawili hao walipoingia katika mgogoro wa ndoa yao hali iliyosababisha mume wa Flora, Emmanuel Mbasha kufikishwa mahakamani kwa kosa la ubakaji. Akizungumza na MTANZANIA jijini Dar es Salaam jana ili kupata ukweli kuhusu taarifa za picha za mtoto huyo ambaye anadaiwa kuwa amezaa na Flora, Mchungaji Gwajima, alisema taarifa hizo ni za uzushi na huenda zinasambazwa na mume wa Flora. Mchungaji Gwajima alikwenda mbali na kusema pamoja na uzushi huo unaosambazwa dhidi yake kwa kuhusishwa katika uhusiano na Flora anamwachia Mungu kila kitu. “Hahaha… si unajua hiyo issue (suala, jambo) ya Mbasha ni ya muda mrefu tu...