Kocha
Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema beki kiraka wa Simba, Erasto
Nyoni atakuwepo kwenye mchezo wa kesho lakini atamkosa Juuko Murshid.
Nyoni ameanza kufanya mazoezi baada ya kupona jeraha la kwenye mguu alilopata mwezi Januari kwenye michuano ya Mapinduzi.
Aussems
amesema Nyoni alifanya mazoezi tangu wiki iliyopita ingawa hakukusafiri
kwenda Algeria ila bado ana nafasi ya kuwa ndani ya kikosi chake kesho.
"Nyoni tulianza naye mazoezi hivyo imani yetu tutakuwa naye kwenye kikosi cha kesho kitakachowavaa AS Vita.
"Kuhusu Juuko bado anahitaji mapumziko mpaka Jumatatu kwa hiyo kwa uhakika Juuko hatakuwepo katika timu," amesema Aussems.
Comments