Washindi wawili wa Jackpot leo wamekabidhiwa million 85 na Kampuni ya Bahati Nasibu ya Premier Bet Tanzania , imekabidhi hundi
hiyo kwa washindi hao wa Jackpot ya soka kwa
Flavian Msigala kutoka Dar es Salaam na Robert Daniel kutoka Mpanda huku kila mmoja atajinyakulia mill 42.5.
Akizungumza na waandishi wa jijini Dar es Salaam,Afisa rasilimali
watu na Meneja utawala Amanda Reuben Kombe amesema kuwa kampuni hiyo
pamoja na Michezo mingine wamekua wakiendesha mchezo wa Jackpot ya soka
kupitia vituo vya mawakala wao na maduka kote nchini Tanzania.
Aidha amesema ikampuni hiyo, imekua ikiendesha shughuli zake kwa
kufuata misingi yote ya kubashiri timu ambayo imewekwa, hivyo amewataka
wananchi kuendelea kubashiri michezo mbalimbali kupitia premier bet ili
kuboresha maisha yao endapo wataibuka washindi na kuachana na propaganda
kuwa washindi hupangwa.
“Kampuni yetu ya Premier Bet huendeshwa kwa kufuata kanuni na sheria
ya michezo ya kubahatisha hivyo nawaomba watanzania waendelee kubashiri
michezo mbalimbali hasa kwenye Jackpot na kutuamini ili tuweze
kubadilisha maisha yao “amesema Amanda.
Kwa upande wake, mshindi wa jackpot hiyo kutoka Mpanda, Robert Daniel
ameipongeza kampuni hiyo kwa kutenda haki ya kuweza kuwapatia fedha
hizo ambazo zitawasidia kuendesha maisha yao.
“Naipongeza sana kampuni hii, kwani imeweza kubadilisha maisha yake,
kutoka mkulima wa mpunga na mfugaji ambapo kwa anaweza kumiliki nyumba
na kuwa mfanyabiashara na kuweza kuendesha maisha yake kwa uhakika ”
amesema Robert
Comments