Kongamano la Maonesho ya Awamu ya Saba ya afya, sayansi na Biashara Jumuiya ya Afrika
Mashariki pamoja na maonyesho ya kimataifa limepangwa kuanza Machi 27
hadi 29 mwaka huu Jijini Dar es Salaam.
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es Salaam leo na Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Muhamad
Kambi wakati akitoa taarifa ya kongamano na maonesho hayo yatayofanyika kwa
siku tatu.
Amesema kuwa
kongamano hilo ni la saba na kwamba lengo ni kubadilishana mawazo kati ya
washiriki ya namna ya kutumia Tekolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama)
katika uendeshaji wa huduma za afya katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika
ya Mashariki (EAC).
“ Maandalizi
yameshafanyika kikao cha mwisho kilifanyika Burundi baada ya miaka kitafanyika
Kenya tunatarajia Samia atalifungua Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julis
Nyerere” amesema Profesa Kambi.
Amebainisha
kuwa kongamano hilo litakwenda sambamba na maonesho ya Tehama huku
akiwasisitiza wananchi kushiriki kupata fursa zitakazowasilishwa.
Amesisitiza
kuwa matumizi ya Tehama kwa kiasi kikubwa yamesaidia katika utoaji tiba,
ufuatiliaji wa magonjwa ya binadamu
pamoja na uendeshaji wa hosptali kwenye ukusanyaji na udhibiti wa mapato.
Kwa upande
wake Katibu Mtendaji wa Tume ya Utafiti katika Afya ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki (EARC), Profesa Gibson Kibiki
amesema kuwa kongamano na maonesho hayo ni mpango mkakati wa miaka 10 na kwamba
utaanza kutumika siku ya ufunguzi.
Profesa
Kibiki amesema kuwa kongamano litaangalia namna bora ya kutumia Tehama kwenye
sekta ya afya ili kufanikisha mpango mkakati huo.
Amefafanua kuwa kauli mbiu ya mwaka huu ni Teknolojia kwa
ajili ya kubadili mifumo ya afya ili kutimiza malengo endelevu ya Umoja wa
Mataifa (UN).
Naye
Mwenyekiti wa Kongamano hilo, Profesa Eligius Lyamuya amesema walipokea mada
200 na kuzichuja kubakia 90 ambapo 10 ni
mtambuka huku 80 zikitarajiwa kuwasilishwa kwa makundi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti
wa Magonjwa nchini (NIMR), Profesa Yunus Mgaya amesema kongamano hilo
litashirikisha nchi sita wanachama wa EAC
na kwamba wananchi wataofika kushuhudia wataona namna Tehama
inavyotumika kwenye sekta hiyo.
Comments