Skip to main content

KCB BANK TANZANIA BIASHARA CLUB YAFANYA SEMINA ARUSHA

Benki ya KCB Tanzania  imefanya juhudi za mahususi za
kuwaleta wadau kujadiliana jinsi ya kutatua baadhi ya changamoto na
kupata njia muafaka za kuendeleza sekta ya utalii nchini

Benki ya KCB Tanzania imefanya kongamano la kwanza la Biashara Club kwa
mwaka 2019 jijini Arusha baada ya kuandaa kongamano kama hilo jijini Mwanza
mwishoni kwa mwaka 2018. 

Pichani ni Bi. Christine Manyeye,Mkuu wa Idara ya Masoko na Mahusaino akijibu maswali kutoka kwa wafanya biashara wa jijini Arusha katika warsha ya Biashara Club iliyofanyika Mt. Meru Hotel tarehe 05 Machi 2019. Semina hiyo iliyohudhuriwa na wafanyabiashara zaidi ya 250 iliwajumuiasha wadau mbali mbali katoka sekta ya utalii wakiwemo Tanzania National Parks Agency (TANAPA), Tanzania Revenue Authority (TRA), Tanzania Association of Tour Operators (TATO) and East Africa Business Council (EABC) kwa nia ya kujadiliana jinsi ya kutatua baadhi ya changamoto na kupata njia muafaka za kuendeleza sekta ya utalii nchini.

Zaidi ya kutoa elimu ya usimamizi wa fedha,uendeshaji wa biashara na sheria za
kodi, KCB Biashara Club pia inawawezesha wafanyabiashara kupanua wigo wa biashara
zao kwa kuwakutanisha na wafanyabiashara wa nje na ndani ya nchi.

Tangu kuzinduliwa kwake, KCB Biashara Club imeendelea kuonyesha dhamira
yake ya kukuza biashara katika seckta ya SME kwa kutoa huduma bora za kibenki
kwa wafanyabiashara wadogo na wakati yaani (SME) pamoja na kuwaonyesha
mbinu za kukuza mitaji ya shughuli zao za kibiashara.


Pichani ni Nd. Ernest Jackinda, Afisa Masoko wa TANAPA akiongea na wageni waalikwa katika warsha ya Biashara Club iliyofanyika Mt. Meru Hotel tarehe 05 Machi 2019. Semina hiyo iliyohudhuriwa na wafanyabiashara zaidi ya 250 iliwajumuiasha wadau mbali mbali katoka sekta ya utalii wakiwemo Tanzania National Parks Agency (TANAPA), Tanzania Revenue Authority (TRA), Tanzania Association of Tour Operators (TATO) and East Africa Business Council (EABC) kwa nia ya kujadiliana jinsi ya kutatua baadhi ya changamoto na kupata njia muafaka za kuendeleza sekta ya utalii nchini.
Biashara Club jijini Arusha lilifanyika Mt. Meru Hotel tarehe 05 Machi 2019
na lilikuwa na lengo mahususi la kukutanisha wadau mbali mbali katika sekta ya
utalii wakiwemo wafanyabiashara. Kongamano hilo lilifanyika katika sehemu
mbili ambapo sehemu yakwanza ilikuwa mahususi kwa wateja wa Benki ya KCB
wapatao 250, huku sehemu ya pili ikiwa ni jukwaa la wazi kwa wakazi wengine wa
Arusha kupata elimu ya huduma za kibenki kutoka kwa wataalam wa Benki ya
KCB.
Akizungumza wakati wa kufungua semina hiyo, Mkuu wa Masoko na Mahusiano, Bi.
Christine Manyenye alisema Benki ya KCB imefanya juhudi za mahususi za
kuwaleta wadau kama Tanzania National Parks Agency (TANAPA), Tanzania
Revenue Authority (TRA), Tanzania Association of Tour Operators (TATO) and East
Africa Business Council (EABC) kwa nia ya kujadiliana jinsi ya kutatua baadhi ya
changamoto na kupata njia muafaka za kuendeleza sekta ya utalii nchini.
Pichani ni  Nd. Masika Mukule, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Masuala ya Kibenki akiongea na wageni waalikwa wakati wa maongezi ya ana kwa ana katika warsha ya Biashara Club iliyofanyika Mt. Meru Hotel tarehe 05 Machi 2019. Semina hiyo iliyohudhuriwa na wafanyabiashara zaidi ya 250 iliwajumuiasha wadau mbali mbali katoka sekta ya utalii wakiwemo Tanzania National Parks Agency (TANAPA), Tanzania Revenue Authority (TRA), Tanzania Association of Tour Operators (TATO) and East Africa Business Council (EABC) kwa nia ya kujadiliana jinsi ya kutatua baadhi ya changamoto na kupata njia muafaka za kuendeleza sekta ya utalii nchini.

Kwa upande wake Meneja wa Tawi, KCB Bank Arusha, Bi. Judith Lubuva
aliwapongeza wafanya biashara, wadau na wakazi wa Arusha kwa kuhudhuria
kongamano. Aliongeza kwamba kongamano hilo limefanyika kwa wakati muafaka
ambapo sekta ya utalii inaendelea kuimarika katika kanda ya kaskazini na
Tanzania kwa ujumla.

Naye Abdul Juma, Mkuu wa Kitengo cha Wafanyabishara Wadogo na wa Kati (SME)
aligusia fursa tofauti zinazoletwa na Biashara Club zikiwemo kuwakutanisha
wafanya biashara mbali mbali wa nje na ndani ya nchi, kupanua wigo wa masoko
kupitia safari za pamoja kwenda nchi kama China, Malaysia na Afrika Kusini.

Juma aliwahakikishia wadau kwamba KCB Bank ina dhamira ya kuinua sekta ya
utalii kwa kuitambulisha Tour Operator Account inayowezesha malipo ya
kieletroniki pamoja na kuwana faida zingine zikiwemo huduma kwa njia ya
mtandao kuwa bure na kutoa pesa bure.
Akiongea katika warsha hiyo, mwakilishi kutoka Mamlaka ya Mapato (TRA), Mr.
Ombeni Urio aliyekuwa mshauri wa masuala ya kodi, alisisitiza umuhimu wa
wafanya biashara hao kufuata kanuni za kodi. Aliipongeza Benki ya KCB kwa
kumualika ili aweze kutoa elimu hiyo ambayo ilikuwa inahitajika kwa sana.

Benki ya KCB inatajwa kuwa ni kubwa zaidi Afrika Mashariki na Kati iliyoanzishwa mwaka
1896 kisiwani Zanzibar. Toka hapo benki imekua na kuenea katika nchi 6 za
Tanzania, Kenya Sudani ya Kusini, Uganda, Rwanda, Burundi na Ethiopia. Leo hii
ina mtandao mkubwa zaidi katika kanda hii ikiwa na matawi 262, mashine za
kutolea fedha (ATM) 962, na wakala 15,000 wanaotoa huduma za benki masaa 24
siku saba za wiki Afrika Mashariki.

Benki ya KCB imesajiliwa katika soko la hisa la Nairobi, Dar es Salaam, Uganda
na Rwanda. KCB Bank Group pia linamiliki kampuni ya bima ya KCB, KCB Capital
na KCB Foundation. Nchini Tanzania, KCB ilifungua milango yake mwaka 1997 na
toka hapo imekuwa mdau mkubwa katika kukuza sekta ya fedha nchini.

Benki ya KCB Tanzania ni mlipa kodi mzuri, mwajiri wa watanzania zaidi ya 300,
inafundisha wafanyakazi wake weledi wa kikazi na pia pale inapotokea nafasi
inapeleka wafanyakazi katika soko la Afrika Mashariki.

Comments

Popular posts from this blog

Thousands of protesters clash with police in Chicago: Chaos in the Windy City as 45 activists arrested and one cop stabbed after demonstrators target NATO

By DAILY MAIL REPORTER Thousands of demonstrators upset with the war in Afghanistan, climate change and the erosion of union rights have raised the intensity of a march in downtown Chicago on Sunday as world leaders assembled for a NATO summit. The protest, one of the city's largest in years, turned violent at the end of an anti-NATO march, where demonstrators confronted Chicago police, pushing against a line of officers several blocks from the lakefront convention center where President Obama hosted a gathering of world leaders. Authorities were seen making arrests one by one and leading individual demonstrators away in handcuffs. After a clash near McCormick Place, Chicago Police Superintendent Garry McCarthy said at a news conference that the protests resulted in 45 people being arrested and four officers suffering injuries - one from a stab wound in the leg. Scroll down for video Clash: Demonstrators try to flee the police as they are move in on them ...

MBINU ZA KUMFIKISHA MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KILELENI KWA HARAKA

Kwa kawaida wanawake wanafikia kilele (mwisho wa utamu wa ngono) kati ya dakika ishirini na saa moja, yaani kwa kifupi inawachukua muda mrefu sana hali inayopelekea mpenzi mvivu kuchoka na ufanyaji wake utakuwa wa “ovyo” hali itakayo kufanya wewe kuishiwa na hamu ya kuendelea. Pamoja na kuchelewa huko ambako kunatokana na utofauti wetu kati ya mwanaume na mwanamke lakini nakumbuka hapo nyuma nilikutana na wanawake 2 waliokuwa ndani ya ndoa na wamezaa lakini hawajawahi kabisa kujua utamu wa tendo hilo alimaharufu kama “kufanya mapenzi”. Natambua kuwa ni ngumu au niseme si wanawake wote ambao wamejaaliwa kimaumbile kwamba wanafanikiwa kufika kileleni zaidi ya mara mbili kila wanapofanya mapenzi/ngono (kumbuka ni kati ya dakika 15 na saa moja hivyo Jibaba hapa awe na uwezo wa kujizuia kwa zaidi ya dk 45) na ikiwa jamaa ni “mzamiaji” basi unaweza ukaondoka na goli 3 ktk mzunguuko mmoja. Lakini kwa nini basi baadhi yao tu ndio wafike kileleni na wengine was...

LEO NI BUNGE LA BAJETI

Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo. -WANANCHI WATAKA IPUNGUZE UKALI WA MAISHA MACHO na masikio ya mamilioni ya Watanzania na wadau wa nje, leo yanaelekezwa Dodoma ambako Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2011/12 itasomwa.Wananchi wengi wamekuwa na shauku ya kujua mwelekeo wa bajeti hiyo hasa katika kipindi hiki ambacho wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha iliyotokana na kupanda kwa bei vyakula na bidhaa za mafuta. Kwa takriban wiki nzima iliyopita, baadhi ya wananchi wamekuwa wakituma ujumbe mfupi wa maandishi kwa simu katika vyombo vya habari, wakiisihi serikali kuhakikisha kuwa bajeti ya mwaka huu inawaondoa katika hali ngumu ya maisha. Bajeti hiyo itakayosomwa bungeni na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo itatangazwa kwa wakati mmoja na bajeti za serikali za nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), katika mtazamo wa kuimarisha mshimakano na umoja wa nchi hizo. Kwa kawaida na mazoea ya muda mrefu, baj...