Makampuni ya simu za mkpononi nchini Tanzania yameridhia kuunda mifumo wezeshi itakayo wawezesha wananchi wanaotumia hidima za smu kupata taarifa mbalimbali za ujasiriamali, biashara, afya na elimu suala ambalo litachochea upatikanaji wa ajira na kukuza kipato.
Makubaliano hayo yanafuatia ripoti ya utafiti ilitolewa leo Jijini Dar es salaam, utafiti uliofanywa na taasisi za REPOA, DTBI,TPSF kuusu namna ambavyo makampuni ya simu za mkononi yanavyoweza kuchochea ukuaji wa shuguli za kiuchumi na hata kuliwezesha taifa kufanikisha Dira ya Maendeleo ya Taifa ifikapo mwaka 2015.
Msimamizi wa utafiti huo, Dk. George Mulamula kutoka DTBI amesema tafiti inaonyesha uwezo mkubwa ambao ukitumika na makampuni hayo utawezesha taifa kukuza ajira hususan kwa wanawake na vijana huku wakizingazia namna ambavyo watawafikia watu wa vijijini.
Comments