Skip to main content

RC Makonda :Awaomba wantanzania kuonesha uzalendo kwa kuishangilia Taifa Stars

BAADA ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuwa imetaja Kamati maalum ya wajumbe 14 kwa ajili ya kuisaidia timu ya taifa, Taifa Stars ifuzu fainali za kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON)  
zitakazofanyika kuanzia Juni 21 hadi Julai 19 mwaka huu nchini Misri.

kamati hiyo inayoongozwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ambaye ni mwenyekiti na katibu ni Mhandisi Hersi Said imesema kuwa jukumu kubwa la kamati hiyo ni kuhakikisha timu hiyo ya taifa inapata ushindi katika mchezo wake wa mwisho wa kundi L kuwania tiketi hiyo ya AFCON dhidi ya timu ya taifa ya Uganda (Uganda Crane) katika mchezo utakaochezwa uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam Machi 24.


Kikosi cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars tayari kimeingia kambini  katika 
hoteli ya Bahari Beach iliyopo Kunduchi mjini Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wa mwisho wa Kundi Lkufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika baadaye mwezi huu.

Akizungumza na waandishi wa habri jana Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alisema 
Taifa Stars watakuwa wenyeji wa Uganda,The Cranes Machi 24, mwaka huu Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam katika mchezo wa mwisho waKundi L kufuzu AFCON Juni 2019 nchini Misri.

Alisema  Stars inahitaji ushindi tu katika mchezo huo wa mwisho ili kufuzu AFCON ya pili kihistoria, huku ikiombea matokeo mabaya Lesotho mbele ya Cape Verde mjini Praia katika mchezo mwingine wa mwisho wa Kundi L.

"Timu hii ni watanzania wote na hivyo tumekutana hapa kwa lengo moja tu la kueleza kuwa kila mtanzania anawajibu wa kuonesha uzalendo wa nchi yake na hivyo tungependa kusema kuwa watanzania waoneshe mapenzi katika mchezo huu muhimu,"alisema Makonda.


Kwa upande wa timu ya Uganda tayari imejihakikishia kucheza AFCON ya Juni nchini Misri baada ya kufikisha pointi 13, wakati Lesotho inayoshika nafasi ya pili kwa pointi zake tano sawa na Tanzania na Cape Verde yenye pointi nne zote zina nafasi ya kuungana na The Cranes.


Timu mbili katika msimamo huo kufuzu kutoka kundi hilo na kama Lesotho itaifunga Cape Verde basi hata Taifa Stars ikiifunga Uganda haitafuzu kwa sababu katika mechi mbili dhidi ya Mamba ilitoa sare na kufungwa ugenini. 


Pamoja na kwamba imekwishafuzu, lakini Uganda inayofundishwa na Mfaransa, Sebastien Desabre imepania kutopoteza mechi hiyo na imepanga kuweka kambi yake mjini Ismailia nchini Misri .

Kikosi cha Taifa Stars kilichoingia kambini  kinaundwa na makipa; Aishi Manula (Simba SC), Aaron Kalambo (Tanzania Prisons), Metacha Mnata (Mbao FC) na Suleiman Salula (Malindi SC).

Mabeki; Hassan Kessy (Nkana FC - Zambia), Gardiel Michael (Yanga SC), Kelvin Yondan (Yanga SC), Vincent Philipo (Mbao FC), Ally Mtoni ‘Sonso’ (Lipuli FC), Andrew Vincent ‘Dante’ (Yanga SC), Kennedy Wilson (Singida United) na Aggrey Morris (Azam FC).

Viungo;  Feisal Salum (Yanga SC), Jonas Mkude (Simba SC), Himid Mao (Petrojet FC - Misri), Mudathir Yahya (Azam FC), Shiza Kichuya (ENPPI - Misri), Simon Msuva (Difaa El Jadida – Morocco) na Farid Mussa (Tenerife B).

Washambuliaji; Yahya Zayd (Ismailia - Misri), Shaaban Iddi Chilunda (CD Izara – Hispania), 
Rashid Mandawa (BDF XI - Botswana), Thomas Ulimwengu (JS Saoura - Algeria), John Bocco (Simba SC)na Mbwana Samatta (KRC Genk – Ubelgiji). 

Naye ameita kikosi imara ambacho kinaundwa na  makipa; Denis Onyango (Mamelodi Sundowns), Jamal Salim (El Merreikh), Charles Lukwago (KCCA FC) na Nicholas Sebwato (Onduparaka FC).

Mabeki; Isaac Isinde (Kirinya Jinja SS), Murushid Juuko (Simba SC), Timothy Awanyi (KCCA FC),
Denis Iguma (Kazma FC), Nicholas Wadada (Azam FC), Musitafa Mujuzi (Proline FC), Godfrey Walusimbi (Gor Mahia) FC, Isaac Muleme (Haras El Hodood), Joseph Ochaya (Lusaka Dynamo), Hassan Wasswa (El 

Geish), Khalid Aucho(Huru), Ibrahim Saddam Juma (KCCA FC), Tadeo Lwanga (Vipers SC), Opondo Moses( Vendsyssel) na Allan Kateregga (Cape Town City).

Washambuliaji ni Faruku Miya (Gorica ), Moses Waisswa (Vipers Sc), Yunus Sentamu (FK Tirana), Martin Kizza (Sc Villa Jogoo), Allan Kyambadde (KCCA FC), Emmanuel Okwi (Simba SC), Edrisa Lubega (SV Ried), Derrick Nsibambi 

(Smouha),Patrick Kaddu (KCCA FC), William Luwagga Kizito (FC Bate Borisov) na Yasser Mugerwa (Fasil Kenema).

Mwishoo.

Comments

Popular posts from this blog

MBINU ZA KUMFIKISHA MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KILELENI KWA HARAKA

Kwa kawaida wanawake wanafikia kilele (mwisho wa utamu wa ngono) kati ya dakika ishirini na saa moja, yaani kwa kifupi inawachukua muda mrefu sana hali inayopelekea mpenzi mvivu kuchoka na ufanyaji wake utakuwa wa “ovyo” hali itakayo kufanya wewe kuishiwa na hamu ya kuendelea. Pamoja na kuchelewa huko ambako kunatokana na utofauti wetu kati ya mwanaume na mwanamke lakini nakumbuka hapo nyuma nilikutana na wanawake 2 waliokuwa ndani ya ndoa na wamezaa lakini hawajawahi kabisa kujua utamu wa tendo hilo alimaharufu kama “kufanya mapenzi”. Natambua kuwa ni ngumu au niseme si wanawake wote ambao wamejaaliwa kimaumbile kwamba wanafanikiwa kufika kileleni zaidi ya mara mbili kila wanapofanya mapenzi/ngono (kumbuka ni kati ya dakika 15 na saa moja hivyo Jibaba hapa awe na uwezo wa kujizuia kwa zaidi ya dk 45) na ikiwa jamaa ni “mzamiaji” basi unaweza ukaondoka na goli 3 ktk mzunguuko mmoja. Lakini kwa nini basi baadhi yao tu ndio wafike kileleni na wengine was...

Uganda Police issue fresh terror alert

  By Chris Kiwawulo, The Police have issued a fresh terror alert against a possible attack on Uganda by four terrorists from Kazakhstan. Police spokesperson Judith Nabakooba “We have received a security notification in form of an orange notice of four terrorists originating from Kazakhstan who are planning to travel to foreign countries in order to commit attacks and participate in hostile acts,” Police spokesperson Judith Nabakooba said in a statement on Monday. Nabakooba named the four active members of radical organizations as; Nassiruauly Kairat, Umurzakov Marat Eskendirovich, Kovtun Denis Valerevich and Mazhibayen Alimzhan Akhlazhanovich. By press time, a search on the international web has not yielded anything on the named persons.Last evening, police said that in collaboration with other security agencies vigilance has been stepped up to avert the terrorists’ evil plans. Police have in the past issu...

Poland’s GROM special services mastermind found dead

Brigadier General Slawomir Petelicki, responsible for the formation of the GROM special services unit in the 1990s, was found dead at his apartment, Saturday, with bullet wounds to the head. Sławomir Petelicki, 1946-2012. Photo: Archive/PAP/Radek Pietruszka Police spokesman Maciej Karczynski informed that Petelicki’s body was found by his wife in the garage of his Warsaw apartment on Saturday. He was 65. Primary investigations point to suicide as the cause of death. It is expected that prosecutors will decide on an investigation into Petelicki’s death on Monday. After examining the scene of the incident, “the body of General [Petelicki] has been taken to a forensic laboratory, although a post-mortem will probably take place on Monday,” prosecutor Katarzyna Calow-Jaszewska from the Warsaw District Prosecution told the PAP news agency. “He was a tough man, a brilliant soldier and commander,” Colonel Krzysztof Przepiorka, head of the ...