Pichani ni Mkurugenzi wa kituo cha uwekezajiji (TIC) Geofrey Mwambe, akizungumza na waandishi wahabari pamoja na maafisa wa kituo hicho leo jijini Dar es slaam.
WATANZANIA wametakiwa waepukana na dhana ya kuwa wawekezaji
ni kutoka nje ya nchi pekee bali nao wanapaswa kuwekeza kwa kutumia
fursa zilizopo kwani mazingira ya uwekezaji ni mazuri.
Kituo Cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimezitaka taasisi za Serikali na
sekta binafsi kushirikiana kikamilifu katika kukuza sekta ya uwekezaji
hapa nchini ili kusaidia kuondoa wimbi la ukosefu wa ajira kwa vijana.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam Wakati akitoa taarifa
ya kituo hicho kutoka kuwa chini ya Usimamizi wa Wizara ya viwanda na kuwa Wizara
ndani ya Ofisi ya Waziri Mkuu Mkurugenzi Mtendaji Bw. Geofrey Mwambe amesema kuwa
kwa sasa kazi yao kuu itakuwa ni kuratibu maswala mbalimbali ya kuboresha uwekezaji
ndani na nje ya nchi.
“Umma wa watanzania unatakiwa kutambua kuwa Mheshimiwa Rais Magufuli anafanya kila
jitihada kuhakikisha kuwa uwekezaji Tanzania unakua hivyo taasisi za serikali tunapaswa
kumuunga mkono kwani kwa sasa ameshafanya vya kutosha imebakia sehemu yetu,"alisema Mwambe.
Bw. Mwambe alisema kuwa uwepo wa Wizara hiyo mpya ambayo tayari inawaziri
wake itasaidia upatikanaji wa masoko na uongezwaji thamani wa bidhaa ambapo
wawekezaji wa ndani na nje ya nchi wataendelea kuiamini Tanzania na uwekezaji
wake kukua zaidi.
Aidha amesema kuwa mtu yeyote anayetaka kuwekeza asisite kuzifuata Mamlaka
mbalimbali ikiwemo za mkoa na Wilaya kwani zipo kisheria kwa lengo la
kuwahudumia na kutatua kero zote wanazokumbana nazo katika shughili za uwekezaji.
TIC kilipoaanzishwa kinajipambanua kuwa,kilianzishwa kwa lengo la kuhamasisha,
kuwavutia na kuwezesha uwekezaji wa ndani na nje ya nchi ili kukuza sekta
binafsi na kuinua uchumi wa taifa lakini pia kuishauri serikali juu ya masuala
ya uwekezaji nchini ambapo pia imeelezwa kuwa uchumi wa Tanzania unakua kwa kasi
kubwa na kwa sasa inashika nafasi ya tano kati ya mataifa 10 duniani yenye
uchumi unaokuwa kwa kasi
Mkurugenzi Mwambe amesema ni vyema wawekezaji wa hapa nchini wakajenga uhusiano
mzuri na wawekezaji kutoka nje ya nchi kwani ni jambo ambalo litasaidia kuendelea
kukuza maendeleo ya uchumi wa viwanda
Hata hivyo ametoa wito kwa watanzania kuwa wazalendo na nchi yao kwa kuijengea
sifa wawapo nje ya nchi ili kukuza Mahusiano mazuri ambayo yatawavutia wawekezaji
na kukuza uchumi wa Taifa.
Kituo cha uwekezaji Tanzania TIC kimewataka watanzania kutumia fursa ya kujinufaisha
na ujio wa wawekezaji kutoka nje ya nchi ili kwa pamoja waweze kujenga na kuimarusha
uchumi wa nchi.
Ata hivyo imetaja kuwa serikali haiwezi kufanikisha dira ya Uchumi wa Kati
wa Viwanda , kama Sekta binfsi haiko imara,hivyo kuimarisha sekta binafsi
ya Tanzania itasaidia zaidi kuchochea ukuaji wa uchumi.
Mkurugenzi huyo Mtendaji wa kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) alisema
wamekuwa na malengo mazuri ya kutangaza fursa ya uwekezaji,ili
kushawishi na kuvutia wawekezaji kuja kuwekeza nchini pamoja na kushiriki
kongamano ya biashara na uwekezaji.
TIC imeongeza kuwa serikali inaendelea kuweka mazingira rafiki kwa
wawekezaji wa ndani na nje,pamoja na kutoa elimu kwa wajasiliamali
wa hapa nchini,ili watambue fursa zilizopo, ambapo hatua hiyo itasaidia
kupata watanzania wengi mabilionea kwa siku zijazo.
Comments