WAKATI jamii mbali mbali duniani wakiendelea kutumia mfumo wa teknolojia (TEHAMA) imeelezwa kuwa maarifa zaidi yataendelea kuongezeka kutokana na kuutumia mfumo huo.
WANAFUNZI WA CHUO CHA USIMAMIZI WA FEDHA (IFM) WAKIFATILIA UZINDUZI WA ASASI YA HIFADHI YA JAMII ULIODHAMINIWA NA PSPF. NI MOJA YA TUKIO LA ZAMANI.
Yapo mafanikio na moja ya mifano ya mafanikio ya Tehama ni kubuniwa kwa mfumo wakufuatilia madereva wanaoendesha mwendo wa haraka ambapo mfumo huo umesaidia kupunguza ajali ikilinganishwa na kipindi cha nyuma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasialiano) Dk.Jim Yonazi amesema Tehama imesaidia kutatua matatizo mengi ya kijamii na kiuchumi.
Dk. Yonazi aliyasema hayo juzi wakati wa semina ya siku mbili juu ya umuhimu wa Tehama katika kujiletea maendeleo iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam.
“Tehama ina mchango mkubwa sana katika maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla hivyo hatunabudi kuhimiza wananchi kutumia Tehama ili kujiletea maendeleo na kutatua changamoto mbalimbali,”amesema
Dk. Yonazi alisema Tehama ikitumiwa vizuri inaweza okoa maisha ya mama mja mzito kwakufuatilia programu mbalimbali za lishe na malezi bora kupitia simu ya kiganjani.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Profesa Tadeo Satta alisema tehama ikitumiwa vzuri huongeza ubunifu na maarifa hivyo aliwataka wananchi kutumia Tehama kujiletea maendeleo.
“Tehama hadi sasa inaendelea kusaidia kuongeza ubunifu na maarifa ambapo wengi wamenufaika ili kufanikisha hilo IFM tumeandaa washa ya siku mbili kwa watumishi na wanafunzi wa IFM kama sehemu yakujuzana umuhimu wa Tehama,”amesema
Profesa Satta alisema semina hiyo itawajengea uwezo watumishi wa IFM ikizingatiwa kuwa muongoza mada katika washa hiyo ni mbobevu katika masuala ya Tehama ambaye ni Profesa Henk Sol wa Chuo Kikuu cha Groningen cha nchini Uholanzi.
“Tumekuwa tukibadirishana uzoefu na vyuo vya kimataifa ili kuweza kuleta maendeleo katika Taifa letu kwakuwa ukiwajengea uwezo wanataaluma umeelimisha Taifa zima hususani katika mmatumizi bora ya teknolojia katika kuboresha huduma na ufanisi,”
Naye Muongozaji wa mada mbalimbali zihusuzo Tehama katika washa hiyo Profesa Sol amesema nchi za magaharibi ikiwemo Uholanzi zimepiga hatua kubwa sana kutokana na matumizi ya Tehama.
"ugunduzi wa Tehama ulianzia katika nchi za mabara ya Ulaya na Marekani lakini lakini umekuwepo ukweli kwa watu wake ambao wamechangamkia fursa na wameweza kujiletea maendeleo kikubwa nikuwa wabunifu nakuitumia Tehama kama injini yakujiletea maendeleo."
Comments