UJUMBE wa maofisa wa benki 7 na menejimenti ya Benki ya Posta ya Kenya upo nchini
kwa ziara ya siku tatu kwa ajili yakujifunza namna yakuendesha benki
kibiashara.
Benki ya Posta Tanzania (TPB) imekuwa kimbilio la mabenki
ya serikali ya nchi za Afrika Mashariki na kusini mwa Afrika ambapo baadhi ya
nchi hizo huja nchini kujifunza katika Benki hiyo.
Benki ya Posta Tanzania imejipambanua kuwa imerasimishwa kuwa benki ya
Biashara miaka 3 iliyopita ikijiendesha kwa hisa za aslimia 86 kutoka
serikalini wanahisa wa benki 8%, serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na asilimia
2 kutoka kwa wanahisa wa posta na simu Sacos.
Hayo yamezihirika jana ambapo licha ya ujumbe wa maofisa wa hao 7 awali benki
nyingine iliyokuja kujifunza TPB ni Benki ya Posta ya Botswana iliyokuja mwaka
jana.
Mwenyeji wa ujumbe huo ni Menejimenti ya Benki ya TPB ikiongozwa na Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Sabasaba Moshinge,ujumbe huo upo kwa dhumuni la
kujifunza mambo mbalimbali yakibenki.
“Ujumbe wa Benki ya Posta ya Kenya ipo hapa kwa ajili ya kujifunza
masuala ya kibenki, kwakuwa sisi tupo mbele yao kihuduma, tumekuwa benki ya
Biashara na wao wanataka kuwa Benki ya Biashara lazima wajifunze kwetu na mwaka
jana pia tulipokea ujumbe kama huo kutoka Botswana,”alisema
Moshinge alisema kuwa TPB inatoa huduma zote za kibenki ikiwemo mikopo
wakati Benki ya Posta ya Kenya haitoi huduma ya mikopo zaidi yakuweka amana za
wateja na kuzilinda.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Kenya Anna Karanja, alisema
Benki hiyo ina zaidi ya miaka 100 katika huduma za kibenki na sasa ipo katika
mchakato wa kuwa benki ya Biashara, wamekuja Tanzania kujifunza kutoka kwa
Benki Pacha ya Posta (TPB)
“Tupo hapa kujifunza kutoka kwa ndugu zetu wa TPB kwakuwa wao
wametutangulia kuingia katika mfumo wakuendesha benki kibiashara hatunabudi
kujifunza kutoka kwa watangulizi wetu ,”alisema
Anna alisema kuwa wamechagua TPB kwakuwa kwakipindi kifupi imejitwalia
mafanikio makubwa katika utoaji wa huduma za benki kibiashara hususani Biashara
Mtandao.
Miongoni mwa mambo ambayo ujumbe huo utaangalia ni mfumo mzima wa menejimenti
ulivyo, jinsi yakusimamia uendeshaji wenye tija na faida, bodi inavyoshughulika
na shughuli za kila siku za kibenki na kufahamu umiliki wa hisa ukoje.
Hata hivyo Moshinge alisema Benki hiyo ina mahusiano ya karibu na Beki ya
Posta ya Kenya ambapo zilianzishwa siku moja na mwaka mmoja kipindi cha
iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki kabla haijavunjika.
Comments