CHUO cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kimeliomba Baraza la Taifa la elimu ya
ufundi (NACTE) kuharakisha utoaji wa ithibati ya rasimu mpya ya mtaala
wakufundishia Astashahada na Shahada ya uzamili ya mafunzo ya utawala katika
hifadhi ya jamii.
Makamu Mkuu wa Chuo hicho Dk. Emanuel Mnzava ametoa ombi hilo leo wakati wa makabidhiano ya rasimu ya
mtaala mpya wa masomo ya hifadhi ya jamii kutoka kwa kamati iliyoandaa rasimu
hiyo.
āKumekuwa na hitaji kubwa na pengo katika mtaala unaofundisha masomo ya hifadhi ya jamii kwa sasa, kutokana na ukweli kwamba baadhi ya vipengele havisawiri
mazingira ya Tanzania,āamesema.
Dk. Mnzava amesema kuharakishwa kwa mtaala huo kutasaidia kutatua baadhi
ya changamoto zilizopo katika sekta ya mifuko ya hifadhi ya jamii nchini
kwakuwa itazalisha wataalamu wabobevu watakaoshiriki kutatua changamoto za
sekta hiyo.
Kwaupande wake Kiongozi wa kamati (timu) ambaye ni Kamishina wa Mamlaka ya Bima Dk. Baghayo Saqware amesema kuwa kuna uhitaji wakufanyiwa
marekebisho ya mtaala uliopo ili uwakisi mahitahi ya soko kidunia.
āLengo la huu mtaala nikuongeza rasilimali watu watakaosoma masomo ya
hifadhi ya jamii na mchakato wote umehusisha wadau mbalimbali na wanataaluma
wabobevu kutoka vyuo saba nchini na vyuo vya nje ya nchi,"amesema.
Aidha Dk Saqware amesema mwisho wa programu hiyo itapelekwa NACTE kwa
ajili yakufanyiwa tathimini itakayosaidia NACTE kutoa ithibati itakayo waruhusu
IFM kudahiri wanafunzi.
Hata hivyo Dk. Saqware amesema kuna umuhimu wakufanya tafiti zakutosha
ili kupata hadidu za rejea zitakazosaidia katika ufundishaji ili ziendane na
mazingira ya nchi na kikanda.
āSisi washiriki kutoka vyuo vikuu tunashukuru kushirikshwa katika
mchakato huu natutaendelea kushirikiana na IFM pale mtakapotuhitaji,āamesema.
Aidha Dk. Soud amesema mtaala huo utasaidia sana nautatoa wigo mpana kwa
mtu yeyote kusoma taaluma hiyo hata kwa ngazi ya cheti tofauti na sasa.
Rasimu hiyo ilianza kuandaliwa mwaka 2016 na timu ya wataalamu kutoka
vyuo saba nchini ikiongozwa na Dk. Baghayo Saqware Mkurugenzi Mkuu wawakala wa
Bima, Profesa Godfrey Sansa (Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Aley Soud Chuo
Kikuu Zanzibar (SUZA)
Wengine ni Tumaini Yarumba (Chuo cha Ushirika Moshi),Dk. K.Mashaushi,
Athur Ngasani, Frank Kitende wote wa IFM.
Comments