SOKO la Ilala Boma Jijini Dar es Salaam
linaendesha
zoezi lakuwasajili wafanyabiashara wote sokoni hapo wanao miliki vizimba na
meza nakuwarasimisha katika mfumo wa kanzi data, mfumo huo unatajwa kuwa
muoarobani wa kuvamia soko hilo.
Mwandishi wa gazeti hili
jana alishuhudia wafanyabiashara wakijisajili katika ofisi ya Ofisa Mkuu wa
soko, kukamilika kwa kanzi data hiyo kutasaidia soko hilo kutoa huduma stahiki
na kwa weledi wa hali ya juu na kusaidia katika tathimini ya ujenzi wa soko jipya.
Akizungumza katika soko hilo Ofisa Mkuu wa soko, Seleman Mfinanga alisema Uongozi
wa soko pia
umedhamiria
kuboresha mazingira ya soko hilo kwa kugawa namba kwa ajili ya kuwatambua
wafanyabiashara wa soko hilo.
Mfinanga alisema Uongozi wa soko
hilo chini ya Ofisi ya Mkurugenzi wa
Manispaa ya Ilala ipo katika mpango wakuboresha masoko yake yote likiwemo la Ilala Bora.
Akijibu malalamiko hayo Mfinanga
alikiri kuwepo kwa baadhi ya changamoto zilizoainishwa nakuzitolea ufafanuzi
nanamna zitakavyotatuliwa hivi karibuni.
“Kwa uchakavu wa miundombinu
ninakubaliana nalo, “nikweli mitaro ina kina kidogo , wakati wamvua huibua
tafrani na mafuriko lakini wakati huu wa kiangazi mitaro hiyo huwa safi,”
Mfinanga alisema Kampuni iliyopewa
zabuni yakukusanya taka na ushuru wa soko hilo inajitahidi kadri iwezavyo
tofauti na kampuni iliyopita,kuhusu ushuru sheria inayoongoza soko hilo
inaeleza bayana pasipo ujazo kuwa taka zitalipiwa ushuru wa sh500iwe gunia,
kisafleti au tenga vyote ni sh500 tu.
Mfinanga aliongeza kuwa changamoto
kubwa ya soko hilo nikukokosekana kwa ukuta kiasi kwamba wanashindwa kujua
idadi kamili ya wafanyabiashara sokoni hapo kwakuwa huingia kiholela lakini
ukuta utakapojengwa tatizo hilo litakwisha.
“Gari la usafi hukusanya
taka kila siku saa nne asubuhi, kuna wafanyabiashara wa aina mbili kuna ambao
wana meza na kuna ambao hupanga bidhaa chini, gari ya taka hifika saa 10.00
asubuhi kwa ajili ya kukusanya taka na wafanyabiashara walioweka bidhaa chini
wanalipisha likiondoka wanarudi tena lazima kuwe na uchafu ukipita majira ya
alasiri na jioni,”alisema
Malalamiko mengine yaliyo
ainishwa na wafanyabiashara sokoni hapo kwa shariti la kutoandikwa majina yao
ni pamoja na soko hilo kukosa uongozi wa mwenyekiti , katibu na mweka hazina
wao kama ilivyo kwa masoko mengine.
Akijibu malalamiko hayo
Mfinananga alisema rasimu imekwishaandaliwa na viongozi wa umoja wa
wafanyabiashara wa vitengo mbalimbali sokoni hapo walishiriki katika rasimu
hiyo ambayo hivi karibuni itakuwa moja ya sheria katika sheria ndogondogo za
halmashauri.
“Tumewashirikisha viongozi
wa vitengo na wenyewe wamependekeza kikomo cha uongozi wa uwenyekiti wa soko
nikipindi cha miaka 3 na uwezekano wakuchaguliwa kuongoza kipindi kingine,
rasimu hiyo imefuata michakato na miongozo yote ya sheria inayoongoza
halmashaururi ya manispaa ya Ilala,”
Comments