Beki wa Simba Erasto Nyoni aliumia wakati Simba ikiivaa KMKM katika mechi ya Kombe la Mapinduzi, Visiwani Zanzibar jana.
Kutokana na maumivu Nyoni alikimbizwa hospitali wakati mechi ikiendelea kwa hiyo atakaa nje kwa wiki tatu akiuguza majeraha ya goti.
Awali Daktari wa Simba, Yassin Gembe alisema alikuwa ameona jeraha si kubwa sana ingawa ilitakiwa kufanya vipimo kwanza.
Nyoni ambaye alijiunga na Simba akitokea Azam FC amekuwa sehemu ya nguzo ya ulinzi katika kikosi cha Simba ambacho kimefuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi.
- Get link
- X
- Other Apps
- Get link
- X
- Other Apps
Comments