Wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wamekutana leo jijini Dar es Salaam kwa ajili na kutoa maoni kuhusu muswada wa sheria wa vyama vya siasa.
Akizungumza katika mkutano huo ,Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole, amesema sheria vya vyama vya siasa iliyopo sasa haimpi nguvu Msajili wa Vyama vya Siasa kufanya kazi kwa ufanisi hivyo mabadiliko ya muswada mpya yatasaidia uimara wa vyamavyasiasa na Ofisi ya Msajili kufanya kazi kwa ufanisi.
Amesema ,Mabadiliko hayo yatampa nguvu msajili wa vyama vya siasa kutazama kwa jicho la upole endapo chama kimefanya vizuri na jicho la ukali kwa mamboya hovyo ambayo chama kitafanya
vilevile mabadiliko hayo yatampa nguvu Msajili kuhusika kwenye usajili wa vyama vya siasa, kusimamia chaguzi za vyama vya ndani, kutoa na kufuatiliauwajibikajiwaruzuku.
Amefafanuakuwa sheria inayotumika sasa ni ya mwaka 2010 ni miaka 10 imepita tangu kufanya mabadiliko ya sheria, sisi ni vijana tunatakiwa tutoe maoni na mabadiliko ya sheria mpya ili sheria mpya itakayokuja kutumika isiweze kumbana msajili wa vyama vya siasa pamoja na sisi wanachama,” amesema Polepole.
Ameeleza kuwa kuna vyama vya siasa vimekuwa vikitumia fedha za ruzuku kinyume na utaratibu, hivyo kupitia muswada fedha za umma zitatumika kama zilivyokusudiwa.
Hata hivyo amewataka wanachama wa CCM na wadau wa siasa kutoa maoni yao kuhusu muswada wa sheria wa vyama vya siasa ambao ni rafiki kwa ajili ya maendeleo ya taifa.
Kwa upande wake katibu wa siasa na mahusiano ya kimataifa wa CCM, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga amewataka wanachana wa chama hicho kutoamaoniyaobilawasiwasikuhus u muswada huo.
Comments