Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (katikati) akikagua mradi wa ujenzi wa chumba cha pampu ya maji katika Chuo cha maendeleo ya Jamii Mlale unaogharinu Shillingi Millioni 3 unaosimamiwa na Chuo cha Maendeleo ya Jamii na Ufundi Misungwi katika ziara yake mkoani Ruvuma kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololeti Mgema na Kushoto ni Mkuu wa chuo cha Maendeleo ya Jamii Mlale Luciana Mvula
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (katikati) akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Mlale mkoani Ruvuma wakati wa ziara yake chuoni hapo kujionea Ujenzi na Ukaratabi wa miundombinu mbalimbali kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololeti Mgema na Kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Mlale Luciana Mvula.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (kulia) akikagua mabweni yaliyofanyiwa ukarabati katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Mlale katika ziara yake mkoani Ruvuma katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololeti Mgema na Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Badru Rwegarulira.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na baadhi ya wakufunzi, wafanyakazi na wananfunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Mlale mkoani Ruvuma wakati wa ziara yake chuoni hapo kujionea Ujenzi na Ukaratabi wa miundombinu mbalimbali.
Baadhi ya ya wakufunzi, wafanyakazi na wananfunzi wa wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Mlale wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (hayupo pichani) wakati wa ziara ya Naibu waziri huyo chuoni hapo kujionea Ujenzi na Ukaratabi wa miundombinu mbalimbali.
Moja ya jengo la bweni liliofanyiwa ukarabati katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Mlale mkoani Ruvuma. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amewaagiza watendaji wa Halmshauri zote nchini kutotumia wakandarasi katika kutekeleza miradi inayohusu Wizara bali kutumia mtindo wa 'Force Account' yani mafundi wa kawaida katika kutekeleza miradi hiyo.
Ametoa agizo hilo mkoani Ruvuma wakati alipotembelea na kujionea ukarabati na ujenzi katika Chuo cha Wauguzi Songea na Chuo cha Maendeleo ya Jamii Mlale katika ziara yake ya kikazi mkoani humo. Naibu Waziri huyo amefikia hatua hiyo baada ya kupokea taarifa ya kuanza kwa mchakato wa ujenzi wa baadhi ya madarasa na ukuta wa Chuo cha Waganga mkoani humo ambao ungegharimu zaidi ya Shillingi 900 ambazo fedha hizo zingetumia mtindo wa 'Force Account' zingejenga zaidi madarasa hayo na ukuta.
Dkt. Ndugulile ameongeza kuwa katika zama hizi za Serikali ya Awamu ya Tano itazingatia na kufuatilia matumizi sahihi ya fedha za miradi ya Maendeleo na yeye kama Naibu Waziri ataisimamia kwa karibu Miradi hiyo. Amesisitiza kuwa ujenzi wote wa miradi utakaohusu Idara Kuu Maendeleo ya Jamii utazingatia utaratibu wa 'Force Account' na kibali cha wakandarasi kitatolewa na Mawaziri pekee na sio vinginevyo.
"Niseme tu ni marufuku kutumia wakandarasi katika kutekeleza miradi inayohusu Wizara hii niliyopo labda muyafanye haya wakati mimi sipo" alisisitiza Dkt. Ndugulile. Akitoa taarifa ya ujenzi na ukarabati wa Chuo cha Wauguzi Songea Kaimu Mkuu wa Chuo hicho Dkt Geofrey Mdodo amesema Chuo kinakabiliwa na changamoto za miundombinu na upungufu wa wakufunzi ambapo mpaka sasa kuna wakufunzi saba wanaofundisha jumla ya wanafunzi 105.
Wakati huo huo Naibu Waziri Ndugulile ametembelea na kukagua ujenzi na ukarabati wa madarasa na mabweni na mradi wa maji katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Mlale Songea. Dkt. Ndugulile ameongeza kuwa Serikali imedhamiria kuzalisha wataalam katika kuwaletea Maendeleo hasa wataalam wa Maendeleo ya Jamii ikiwa ni kada muhimu katika mstakabali wa Maendeleo ya taifa letu.
Dkt. Ndugulile amewasihi wataalam wa Maendeleo ya Jamii kuamsha ari ya wananchi katika shughuli za Maendeleo kushirikiana na Serikali katika kutekeleza miradi ya Maendeleo. "Niseme Kada hii ya Maendeleo ya Jamii ni muhimu Maafisa Maendeleo ya Jamii tuamshe ari na Jamii wajue jukumu la kujiletea Maendeleo ni la wananchi na Serikali na sio Serikali pekee" alisisitiza Dkt. Ndugulile.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololeti Mgema amemuahidi Naibu Waziri kusimamia uendeshaji wa Chuo hivyo vilivyopo katika Wilaya yake kwa ukaribu.
Akitoa taarifa miradi ya ukarabati wa madarasa, mabweni na ujenzi wa miradi wa maji katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Mlale Mkuu wa Chuo hicho Luciana Mvula amesema kuwa ukarabati wa Ofisi kwa mwaka 2016/2017 uligharimu shillingi millioni 91, ukarabati wa mabweni na vyoo umegharimu shillingi Millioni 152 na ujenzi wa mradi wa kusukuma maji uliogharimu shillingi millioni 3.
Wakizungumza baadhi ya wananchuo na Watumishi wameiomba Serikali kuongeza wakufunzi na wafanyakazi katika Chuo hicho ili kuendana na mabadiliko ya mtaala uliopo. Naibu Waziri Dkt. Faustine Ndugulile yupo mkoani Ruvuma kwa ziara ya Siku mbili kufuatilia utekelezaji katika Sekta ya Afya na Maendeleo ya Jamii nchini.
Comments