Rapper kutoka Tanzania Ambwene Yesaya alimaarufu AY, afunguka mwanzo mwisho kuhusu historia yake. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Msanii huyo amefunguka kuanzia kuitwa Ambwene Yesaya hadi AY.
Pia ameongelea kuanzia safari ya maisha yake kwa ujumla na kusema:-
“Heri ya Mwaka Mpya Ndugu zangu.Leo ngoja niwaambieni story kwa ufupi jinsi Ambwene baadaye akawa AY alivyokuja kupambana na maisha Jijini Dar Es Salaam.
Nilikuja Dar mwaka 1999 kwa msukumo wa Ndugu yangu @gzingalize ambaye tulikuwa tunasoma wote Ifunda Technical School IRINGA.
Nilikuja Dar nikiwa na ndoto moja tu ya kufanikiwa kupitia kipaji changu cha Muziki. Nilipofika sehemu niliyoanza kuishi ni kwenye Container hili hapo nyuma na ndio sehemu nilikaa kwa kipindi kirefu kabla sijapewa hifadhi kwa familia ya @gzingalizehalafu nikahamia kwa kina @kingcrazy_gk.
Container hili lilikuwa linatumiwa na mafundi wa kushona nguo. Hivyo kila siku ilikuwa ni lazima niamke saa kumi na mbili asubuhi kabla Mafundi hawajafika. Pia ilibidi kuoga ilikuwa kutembea mpaka MNAZI MMOJA kwenye mabafu ya Jumuiya yaliyoko pale ya kulipia.
Mwisho wa siku ilikuwa lazima ndoto itimie bila kujali mazingira husika. NI MUHIMU KUSHUKURU KWA KILA JAMBO MUNGU ANALOKUBARIKI NALO NA KUWEKA BIDII KWENYE NDOTO ZAKO PERIOD!!.. 📸 @shaffieweru 😊
Comments