Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Mhe. Jokate Mwegelo ameipongeza klabu ya Simba kwa ushindi mnono wa goli 3-0 dhidi ya waarabu kutoka Algeria, JS Saoura .
Kwenye pongezi hizo, DC Jokate amewatumia pongezi kwa ushindi huo, huku akitumia jina la Watanzania.
“Kama shabiki wa Yanga nawapongeza Watanzania wenzetu kwa ushindi huu muhimu Mungu Ibariki Tanzania.“ameandika Jokate kwenye ukurasa wake wa Twitter .
DC Jokate ni shabiki wa kutupwa wa Klabu ya Yanga. Jana simba ilipata ushindi huo muhimu kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Klabu Bingwa barani Afrika.
Comments