Mchezaji wa West Ham Andy Carroll, mwenye umri wa miaka 30, ameibuka na kuwashangaza wengi kwa kupigiwa upatu kuichukua nafasi ya mshambulizi wa Tottenham kutokana na kujeruhiwa kwa wachezaji wa timu hiyo.’ (Sun)
Eden Hazard hatojiunga na Real Madrid mwezi huu lakini mchezaji huyo wa miaka 28 anataka kukataa maombi mengine yoyote na ahamie katika klabu hiyo bingwa wa Uhispania mwishoni mwa msimu. (Marca, kupitia Mirror)
Chelsea inatarajiwa kukamilisha usajili kwa mkopo wa mshambuliaji wa Juventus Gonzalo Higuain, mwenye umri wa miaka 31, huku naye mlinzi Emerson Palmieri, mwenye miaka 24, huenda akavuka upande wa pili kwa thamani ya £15m. (Star)
Higuain anatarajiwa kuwasili London kesho Jumanne kukamilisha uhamisho wake kutoka Juventus kwenda Chelsea.(Express)
Kocha wa Milan Gennaro Gattuso, aliyetarajia kuwa na Higuain kwa mkopo msimu huu, anasema anakubali uamuzi wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina kuondoka. (Marca)
Juventus inakaribia kufikia makubaliano ya uhamisho kwa mkopo kwa mlinzi wa Manchester United Matteo Darmian, mwenye umri wa miaka 29. (Guardian)
Mchezaji wa kiungo cha mbele wa timu ya taifa ya Colombia James Rodriguez, mwenye umri wa miaka 27, anatarajiwa kukataa nafasi ya uhamisho kwenda Arsenal na atasalia kwa mkopo Bayern Munich hadi ‘angalau’mwisho wa msimu. (ESPN)
Chelsea imewasilisha ombi la kuchelewa kwa mchezaji wa kiungo cha kati wa Barcelona Ilaix Moriba, aliye na miaka 16, ambaye pia Manchester City inamtaka. (Sport)
Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp ameashiria kwamba huenda hatosajili wachezaji wowote mwezi huu, licha ya wachezaji wa kiungo cha ulinzi kujeruhiwa. (Liverpool Echo)
Mkuu wa Monaco, Thierry Henry huenda akakabiliana na iliyokuwa klabu yake Arsenal, kumwania winga wa Atletico Madrid Gelson Martins, mwenye umri wa miaka 23. (O Jogo, kupitia Express)
Mchezaji wa kiungo cha kati wa Leicester Adrien Silva, aliye na miaka 29, anasubiria meneja Claude Puel kuidhinisha uhamisho kwa mkopo kwa timu ya Ufaransa Bordeaux. (L’Equipe, kupitia Leicester Mercury)
Mlinzi wa Porto Eder Militao, ambaye amehusishwa na uhamisho kwenda Manchester United, hatoondoka Ureno mwezi huu na maajenti wa mchezaji huyo mwenye miaka 21 wameashiria uwezekano wa uhamisho kwenda Uhispania katika msimu wa joto. (Manchester Evening News)
Mchezaji wa kiungo cha mbele wa Aston Villa Jonathan Kodjia anatakiwa na klabu aliyokuwa akiichezea Angers, lakini hakuna ombi lililowasilishwa kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 29. (Birmingham Mail)
Aliyekuwa naibu kocha wa Jurgen Klopp, Zeljko Buvac amoendoka rasmi Liverpool baada ya kuafikiwa makubaliano ya mkataba wake. (Liverpool Echo)
Chelsea imewauliza mabingwa wa la Liga Barcelona kuhusu kumnunua mchezaji wao anayedaiwa kuwa na thamani ya £100m kutoka Brazil Philippe Coutinho, 26. (Sunday Express).
Uhamisho wa mkopo wa mshambuliaji wa Juventus Gonzalo Higuain kuelekea Chelsea utamweka raia huyo wa Argentina kuwa miongoni mwa wachezaji wanaolipwa kitita kikubwa katika klabu hiyo cha £270,000 kwa wiki.
Manchester City huenda ikamnunua kwa mkopo kiungo wa kati wa Schalke Sebastian Rudy ,28, (Sun on Sunday).
Mchezaji wa zamani wa Man United Paul Scholes anatarajiwa kuwa mkufunzi mpya wa klabu ya Oldham (telegraph).Mshambuliaji wa Stoke na Uhispania Bojan Krkic, 28, ameanza mazungumzo ya kutaka kuhamia katika ligi ya Marekani ya MLS ambapo atajiunga na klabu ya New England Revolution, ambayo hufunzwa na aliyekuwa kocha wa Blackburn Brad Friedel. (Sun on Sunday).
Mshambuliaji wa Paris St Germain na Ufaransa Kylian Mbappe, 20, anasema kuwa huenda akavutiwa na uhamisho wa kuelekea Real Madrid katika siku za usoni. (AS)
Mkufunzi wa klabu ya Tottenham Mauricio Pochettino anasema kuwa klabu hiyo huenda ikampata mchezaji atakayeziba pengo lililowachwa na mshambuliaji wa Uingereza Harry Kane katika taasisi yake ya mafunzo ya soka kupitia dirisha la uhamisho. (London Evening Standard)
Mkufunzi wa Arsenal Unai Emery anatumaini ya kufanya usajili wiki hii huku kukiwa na ripoti zinazomuhusisha kiungo wa kati wa Barcelona Denis Suare 25. (Daily Star Sunday)
Chanzo BBC.
Comments