Accra Mwandishi wa habari za upelelezi nchini Ghana amepigwa risasi hadi kufa wakati akiendesha gari kwenda nyumbani
Vyombo vya habari vya ndani vinaripoti kuwa watu wasiojulikana wakiwa katika pikipiki walimpiga risasi Ahmed Hussein-Suale mara tatu katika mji mkuu wa Accra Mwandishi wa habari za upelelezi nchini Ghana amepigwa risasi hadi kufa wakati akiendesha gari kwenda nyumbani, baada ya mwanasiasa kuitisha adhabu dhidi yake.
Kwa mujibu wa BBC, Vyombo vya habari vya ndani vinaripoti kuwa watu wasiojulikana wakiwa katika pikipiki walimpiga risasi Ahmed Hussein-Suale mara tatu katika mji mkuu wa Accra.
Alikuwa ni miongoni mwa wahusika wa shirika binafsi la upelelezi Tiger Eye na alipepeleza rushwa katika ligi ya mpira wa miguu Ghana.
Alikuwa ni miongoni mwa wahusika wa shirika binafsi la upelelezi Tiger Eye na alipepeleza rushwa katika ligi ya mpira wa miguu Ghana.
BBC Afrikan Eye ilifanya makala kuhusu skendo hiyo mwaka 2018 baada ya kupata uchunguzi huo kwa ruhusa ya mwandishi machachari Anas Aremayaw Anas, ambaye anaiongoza Tiger Eye.
Baada ya BBC kurusha makala hiyo, mbunge wa Ghana Kennedy Agyapong alisambaza picha za mwandishi huyo Hussein-Suale na kutaka adhabu dhidi yake.
“Akija hapa mpige”, bwana Agyapong anasema kwenye video iliyochapishwa katika moja ya vyombo vya Ghana “chochote kitakacho tokea nitalipa.”
Kupitia mtandao wa kijamii bwana Anas amesema hawezi kunyamazishwa kimya kwa mauaji ya mwenzake.
Bwana Hussien-Suale alipigwa risasi mbili kifuani na moja shingoni majira ya saa 23:00 siku ya Jumatano usiku, taarifa zinasema.
Imeripotiwa kuwa mwili wake ulipelekwa katika hospitali ya polisi na atazikwa hivi karibuni.
Mwandishi huyo wa habari za upelelezi ameshirikiana na BBC katika taarifa kadhaa ikiwemo upelelezi wa uuzaji wa viungo vya watu kwa ajili ya shughuli za kichawi huko Malawi.
Matukio ya unyanyasaji waandishi wa habari ni ya nadra sana Ghana
Kwa mujibu wa IFJ mara ya mwisho mwandishi kuuawa nchini Ghana ni mwaka 2015.
Comments